Ibn Maajah amesimulia kutoka kwa Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa), ambaye amesimulia:

“Wakati mtu alipokuwa akisimama kuswali wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), macho yake hayatoki miguu yake. Baadaye akafa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Wakati mtu alipokuwa akisimama kuswali, macho yake hayaachi paji lake la uso. Baadaye akafa Mtume wa Allaah (Radhiya Allaahu ´anh). Wakati mtu alipokuwa akisimama kuswali, macho yake hayaachi mahali kilipo Qiblah. Baadaye akafa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na kukazuka fitina. Hapo ndipo watu wakawa wanatazama kuliani na kushotoni.”[1]

´Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa) alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuhusu kugeuka kuliani na kushotoni wakati wa kuswali, akasema:

“Ni wizi ambao shaytwaan huiba kutoka kwenye swalah ya mja.”[2]

[1] Ibn Maajah (1634). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (294).

[2] al-Bukhaariy (751).

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 24/11/2025