Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msichinje isipokuwa musinnah, isipokuwa ikiwa itakuwa vigumu kwenu, basi katika hali hiyo mchinjeni jadha´ah kutoka katika kondoo.”[1]
Ameipokea Muslim.
Hadiyth hii ni dalili kwamba miongoni mwa masharti ya kusihi kwa Udhhiyah ni mnyama kufikia umri unaokubalika Kishari´ah, kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Msichinje isipokuwa musinnah.”
Musinnah ni mnyama mkubwa kiumri:
Katika ngamia ni anayekamilisha miaka mitano.
Katika ng’ombe ni anayekamilisha miaka miwili.
Katika kondoo ni anayekamilisha mwaka mmoja. Huyu anaitwa thaniyy kutoka katika wanyama wanaofugwa.
Lakini miongoni mwa wanyama hoa anabaguliwa kondoo ambapo inajuzu kumchinja akiwa jadha´ah, ambaye amefikisha miezi sita. Dhahiri ya Hadiyth inaonesha kuwa jadha´ah haisihi isipokuwa pale ambapo musinnah imekuwa vigumu kupatikana – kwa kupotea au bei kuwa juu. Hata hivyo wanazuoni wengi wamechukulia jambo hili kuwa linalopendekezwa na wakasema inafaa kuchinja jadha´ah hata kama anapatikana musinnah, kwa kuzingatia dalili nyingine nyingi ambazo pamoja zinathibitisha hilo.
Mtu akinunua mnyama kwa ajili ya Udhhiyah, anaweza kumteua kwa maneno kama vile kusema ”Huyu ni mnyama wa Udhhiyah.” Au kwa kumchinja siku ya ´Iyd kwa nia ya Udhhiyah, hata kama hajatamka chochote kabla ya kuchinja. Ama kumnunua tu kwa nia ya mnyama wa Udhhiyah bila kumteua kwa maneno wala kwa kuchinja, hapa ndipo wanazuoni wametofautiana.
Pindi atakapomteua mnyama huyo, basi kunalazimika hukumu zifuatazo:
1 – Hairuhusiwi kumuuza, kumtoa zawadi wala kumbadilisha mnyama huyo isipokuwa kwa aliye bora zaidi. Na kama mmiliki wake atafariki, basi Udhhiyah hiyo achinjwe kwa niaba yake na warithi wake wachukue nafasi yake katika kula, kumtoa swadaqah na kumtoa zawadi.
2 – Kama mnyama huyo atapata kasoro inayozuia kusihi kwake, kama vile ulemavu wa wazi, ikiwa ni kwa uzembe wake, basi atalazimika kumleta mnyama mwingine salama, na ikiwa ni pasi na uzembe wake, basi atamchinja na atasihi.
3 – Akipotea au kuibiwa, ikiwa ni kwa uzembe wake, basi atalazimika kumrudisha mwingine, na ikiwa ni pasi na kuzembea kwake, basi hana jukumu lolote. Na akimpata mnyama wake baada ya muda wa kuchinja kupita, basi atamchinja kama kawaida na atafanya kama anayechinja katika siku za kuchinja.
4 – Haijuzu kuuza chochote kutoka katika Udhhiyah hiyo.
Hata hivyo mtu aliyepewa zawadi ya nyama ya Udhhiyah au aliyetolewa swadaqah kutoka humo, basi anaweza kuifanya atakavyo – kuuza au kumtoa zawadi – kwa sababu sasa ni mali yake halali. Isipokuwa tu haifai auziane na aliyempa zawadi hiyo au aliyejitolea swadaqah hiyo.
[1] Muslim (1963).
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 24-26
- Imechapishwa: 13/05/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 24-26
Imechapishwa: 13/05/2025
https://firqatunnajia.com/16-hadiyth-msichinje-isipokuwa-musinnah-isipokuwa/