Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّهُ لَيْسَ لَهُ سُلْطَانٌ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ إِنَّمَا سُلْطَانُهُ عَلَى الَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُ وَالَّذِينَ هُم بِهِ مُشْرِكُونَ

“Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na kwa Mola wao wanategemea. Hakika mamlaka yake ni juu ya wale wanaomfanya rafiki na ambao wao wanamshirikisha [Allaah] naye.”[1]

Allaah amemfanya shaytwaan kuwa ndiye mfalme wa yule anayemtawala na akamshirikisha Allaah kwa njia ya shaytwaan. Kila ambaye atafanya yeye kazi yake ni kumfuata mtu katika dini ya Allaah basi amemshirikisha Allaah (´Azza wa Jall) na amemfanya huyu anayemfuata kuwa ni mshirika wa Allaah katika hukumu. Allaah hana mshirika yeyote katika hukumu Zake za kidini na za kilimwengu:

إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ

“Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah. Ameamrisha msiabudu mwengine isipokuwa Yeye pekee.”[2]

Nimekazia maneno katika jambo hili ili wapate kutambua wazushi wenye kuzusha kwamba hawana hoja yoyote katika yale waliyoyazua.

[1] 16:99-100

[2] 12:40

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 26
  • Imechapishwa: 25/07/2019