159. al-Qummiy upotoshaji wake wa tatu wa al-Anfaal

al-Qummiy amesema:

”Ahmad bin Muhammad ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far bin ´Abdillaah, kutoka kwa Kathiyr bin ´Ayyaash, kutoka kwa Abul-Jaaruud, kutoka kwa Abu Ja´far ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ

“Enyi walioamini! Muitikieni Allaah na Mtume anapokuiteni katika yale yenye kukuhuisheni!”[1]

Amesema: “Inamaanisha uongozi wa ´Ali bin Abiy Twaalib. Kwani kumfuata yeye na kumkubali kama kiongozi kunaleta umoja miongoni mwenu na kulinda uadilifu kwenu.”[2]

Allaah amemtakasa Abu Ja’far kutokana na uongo huu na upotoshaji. Angalia jinsi wanavyokusudia kufuta maana za Aayah za Qur-aan na kubatilisha ujumla wake.

Kinachokusudiwa na yale yanayowapa watu uhai ni Uislamu ambao uliletwa na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ukiwa na imani zake, ´ibaadah, maadili, miamala, jihaad, kuamrisha mema na kukataza maovu. Aayah haimaanishi, kwa namna yoyote ile, madai haya ya uongo yaliyobuniwa na huyu Baatwiniy.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajawahi kamwe kuhubiri uongozi huu wa kufikirika uliobuniwa na Ibn Saba´, ambao Baatwiniy na Raafidhwah wakaenda kuufanyia kazi kwa ajili ya kukengeusha sehemu kubwa ya Aayah za Qur-aan kwa sababu yake.

[1] 8:24

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/271).

  • Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 219
  • Imechapishwa: 13/08/2025