Mu´tazilah wana misingi mitano:
1 – Tawhiyd. Maana yake ni kukanusha sifa za Allaah. Wanaona yule anayethibitisha sifa za Allaah ni mshirikina.
2 – Uadilifu. Maana yake ni kupinga makadirio. Wanaona kuamini makadirio ni jeuri na dhuluma, na kwamba ni lazima kwa Allaah kufanya uadilifu.
3 – Kuamrisha mema na kukataza maovu. Wanachokusudia ni kufanya uasi dhidi ya viongozi wa waislamu, pale wanapokuwa na maasi yasiyowafanya kuwa makafiri. Uasi wao wenyewe kama wenyewe ni maovu na hauhusiani chochote na kuamrisha mema.
4 – Ngazi kati ya ngazi mbili. Bi maana kusema kuwa watenda madhambi makubwa wanatoka nje ya Uislamu na hawaingii ndani ya ukafiri. Kuhusu Khawaarij wao wanawahukumu moja kwa moja ukafiri.
5 – Utekelezaji wa matishio. Maana yake ni kwamba yule anayekufa akiwa ni mtenda dhambi kubwa isiyokuwa shirki, basi atadumishwa Motoni milele. Wanaafikiana na Khawaarij kuhusu mafikio yake ya mwisho huko Aakhirah. Tofauti yao wao na Khawaarij kuhusu mtenda dhambi kubwa ni kwamba duniani yuko kwenye ngazi kati ya ngazi mbili. al-Qaadhwiy ´Abdul-Jabbaar, mmoja katika viongozi wao, ametunga kitabu kwa jina “Sharh al-Usuwl al-Khamsah”.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 170
- Imechapishwa: 27/11/2024
Mu´tazilah wana misingi mitano:
1 – Tawhiyd. Maana yake ni kukanusha sifa za Allaah. Wanaona yule anayethibitisha sifa za Allaah ni mshirikina.
2 – Uadilifu. Maana yake ni kupinga makadirio. Wanaona kuamini makadirio ni jeuri na dhuluma, na kwamba ni lazima kwa Allaah kufanya uadilifu.
3 – Kuamrisha mema na kukataza maovu. Wanachokusudia ni kufanya uasi dhidi ya viongozi wa waislamu, pale wanapokuwa na maasi yasiyowafanya kuwa makafiri. Uasi wao wenyewe kama wenyewe ni maovu na hauhusiani chochote na kuamrisha mema.
4 – Ngazi kati ya ngazi mbili. Bi maana kusema kuwa watenda madhambi makubwa wanatoka nje ya Uislamu na hawaingii ndani ya ukafiri. Kuhusu Khawaarij wao wanawahukumu moja kwa moja ukafiri.
5 – Utekelezaji wa matishio. Maana yake ni kwamba yule anayekufa akiwa ni mtenda dhambi kubwa isiyokuwa shirki, basi atadumishwa Motoni milele. Wanaafikiana na Khawaarij kuhusu mafikio yake ya mwisho huko Aakhirah. Tofauti yao wao na Khawaarij kuhusu mtenda dhambi kubwa ni kwamba duniani yuko kwenye ngazi kati ya ngazi mbili. al-Qaadhwiy ´Abdul-Jabbaar, mmoja katika viongozi wao, ametunga kitabu kwa jina “Sharh al-Usuwl al-Khamsah”.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 170
Imechapishwa: 27/11/2024
https://firqatunnajia.com/157-misingi-mitano-ya-mutazilah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)