al-Baatwiniy al-´Ayyaashiy amesema:
“Jaabir amesema: “Nilimuuliza Abu Ja’far kuhusu tafsiri ya maneno Yake Allaah:
وَيُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ
”Allaah anataka athibitishe haki kwa maneno Yake na akate mizizi ya makafiri.”[1]
Abu Ja´far akasema: “Tafsiri yake kwa undani ni kwamba Allaah anataka jambo ambalo bado hajalitekeleza. Kuhusu maneno Yake:
أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ
”… athibitishe haki kwa maneno Yake… ”
inamaanisha kuthibitisha haki ya kzazi chake Muhammad. Na maneno Yake:
بِكَلِمَاتِهِ
”… kwa maneno Yake… ”
inamaanisha ´Ali. Yeye ndiye neno la Allaah kwa maana iliyofichika. Na maneno Yake:
وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ
”… na akate mizizi ya makafiri.”
inamaanisha Banuu Umayyah. Wao ndio makafiri. Allaah akate mizizi yao. Na maneno Yake:
لِيُحِقَّ الْحَقَّ
”… ili athibitishe haki… ”
inamaanisha kuthibitisha haki ya family ya Muhammad wakati atapokuja Mahdiy. Na maneno Yake:
وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ
”… abatilishe batili… ”
inamaanisha Mahdiy. Atapokuja atatokomeza mbali batili ya Banuu Umayyah. Hayo ni katika maneno Yake:
لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ
”… ili athibitishe haki na abatilishe batili ijapo watachukia wahalifu.”[2]
Allaah amtakase Abu Ja’far kutokana na madai haya ya ki-Baatwiniy yasiyo na msingi. Aayah hii ni miongoni mwa Aayah ambazo Allaah alizitaja kuhusu tukio la vita vya Badr na yaliyojiri wakati wa mjadala kati ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baadhi ya Maswahabah wake. Baadhi yao walichukia kukutana na kundi la maadui na walitamani kukutana na msafara wa biashara. Kwa sababu hivyo wanapata ngawira bila mapigano:
كَمَا أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِن بَيْتِكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ لَكَارِهُونَ يُجَادِلُونَكَ فِي الْحَقِّ بَعْدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى الْمَوْتِ وَهُمْ يَنظُرُونَ وَإِذْ يَعِدُكُمُ اللَّـهُ إِحْدَى الطَّائِفَتَيْنِ أَنَّهَا لَكُمْ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيْرَ ذَاتِ الشَّوْكَةِ تَكُونُ لَكُمْ وَيُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ
”Kama alivyokutoa Mola wako kutoka nyumbani kwako kwa haki na hakika kundi miongoni mwa waumini linachukia. Wanajadiliana nawe juu ya haki baada ya kubainika – kana kwamba wanasukumwa kwenda katika mauti nao huku wanatazama. Wakati Allaah alipokuahidini moja kati ya makundi mawili kwamba ni lenu, nanyi mkatamani kuwa lisilo na silaha liwe lenu. Na Allaah akataka aithibitishe haki kwa maneno Yake na akate mizizi ya makafiri, ili athibitishe haki na abatilishe batili ijapo watachukia wahalifu.”
Allaah alikuwa amewaahidi waumini moja kati ya makundi mawili: msafara wa biashara au kundi la maadui. Baadhi yao walikuwa wanapenda kukutana na msafara wa biashara, lakini kwa ujuzi na hekima Yake, Allaah akataka wakutane na maadui. Hii ilikuwa kwa ajili ya kuthibitisha haki – ambayo ni dini Yake – kuipa ushindi na kuifanya ionekane wazi na kuangamiza batili – ambao ni ukafiri – kwa kuwaangamiza maadui Zake makafiri. Ndipo lilipotokea lile ambalo Allaah (Subhaanah) alitaka; mapigano yakatokea kati ya mawalii wa Allaah – Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake – na maadui Wake ambao ni Abu Jahl na viongozi wa kikafiri wa Quraysh. Allaah akampa ushindi Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na jeshi Lake ambapo makafiri walishindwa, sabini wakauawa, na sabini wengine wakakamatwa mateka. Hivyo haki ilidhihiri na batili ikatokomezwa. Hiyo ndio maana ya maneno Yake:
كَمَا أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِن بَيْتِكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ لَكَارِهُونَ
”Kama alivyokutoa Mola wako kutoka nyumbani kwako kwa haki na hakika kundi miongoni mwa waumini linachukia.”
Wahalifu watenda madambi na Raafidhwah Baatwiniyyah wanachukia kwamba ushindi huu ulikuwa wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake na kwamba Allaah alithibitisha haki na kuangamiza batili kupitia yeye na kupitia Maswahabah wake watukufu. Badala yake wamekuja na tafsiri hii batili ya ki-Baatwiniy. Badala yake wakadai kwamba haki ni haki ya watu wa Nyumbani kwa Muhammad badala ya haki ya Allaah. Kwa madai ya uongo na ukafiri wamefanya maneno ya Allaah yanayothibitisha haki Yake na kuwapa ushindi waja Wake kuwa ni ´Aliy bin Abiy Twaalib. Waislamu wa kwanza ambao wanachukizwa na uongo huu wa Baatwiniyyah ni ´Aliy na watu wa nyumbani kwake watukufu. Na wamefanya ambaye atasambaratisha batili ni Mahdiy, ngano iliyotungwa ambayo haijawahi kuwepo na wala haitokuwepo. Wanasema kwamba eti Mahdiy huyu atakuja kuwaangamiza Banuu Umayyah na kufuta dola yao, ambayo ilishapita karne nyingi zilizopita. Kwa mtazamo wa watu hawa ni Banuu Umayyah ndio makafiri na wahalifu, si mayahudi, manaswara, waabudia moto wala wanafiki. Huenda mabwana hawa bandia ndio jeshi la Mahdiy katika masiku yajayo.
[1] 8:7
[2] 8:8 Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/50).
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 217-218
- Imechapishwa: 13/08/2025

Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 217-218
Imechapishwa: 13/08/2025
https://firqatunnajia.com/157-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-nne-wa-al-anfaal/