59 – Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam (150-224)[1]
219 – ad-Daaraqutwniy amesema: Muhammad bin Makhlad ametuhadithia: al-´Abbaas bin Muhammad ad-Duuriy ametuhadithia: Nimemsikia Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam akisema juu ya Hadiyth zinazozungumzia kuhusu Kuonekana, Mahali pa kuwekea miguu, Mola wetu anacheka kwa kukata tamaa waja Wake licha ya mabadiliko Yake ya hali zao yako karibu, Mola wetu alikuwepo kabla ya kuumba mbingu, Moto hautojaa mpaka pale atakapoweka Mola wako (´Azza wa Jall) mguu Wake ambapo utasema: “Tosha, tosha” na Hadiyth nyenginezo mfano wa hizo:
“Hadiyth hizi ni Swahiyh. Wamezipokea waaminifu baadhi kutoka kwa wengine mpaka zikatufikia. Tunaona kuwa ni za haki. Lakini tunapoulizwa ni anaweka mguu Wake namna gani au anacheka namna gani, tunasema kuwa hatuzifasiri na hatujamsikia yeyote akizifasiri.”[2]
Abu ´Ubayd ni mmoja katika wale vigogo wa Ijtihaad na bingwa wa lugha. Inakutosha kwamba Abu Ishaaq bin Raahuuyah amesema:
“Allaah anapenda uadilifu. Abu ´Ubayd ni mjuzi zaidi kuliko mimi, ash-Shaafi’iy na Ahmad.”
Abu ´Ubayd alifariki mwaka 224. Aliandika kitabu ”Ghariyb-ul-Hadiyth” lakini hakujishughulisha kufasiri khabari za sifa. Aliona kwamba hapakuwa na tafsiri kwa mambo hayo isipokuwa kwa mujibu wa muktadha wa kiarabu cha Qur-aan – na Allaah (Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.
[1] Mtunzi wa kitabu amesema katika ufupisho wake “yeye na ash-Shaafi´iy wamezaliwa mnamo 150”.
[2] Mtunzi amepokea masimulizi haya kupitia kwa ad-Daraaqutwniy. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh, kama alivotaja mtunzi wa kitabu katika ufupisho wake. Ibn Mandah ameipokea katika “at-Tawhiyd” (2/96 – mswada) kupitia njia zingine, kutoka kwa ad-Duuriy. Ibn Taymiyyah amesema katika “al-Hamawiyyah”:
”al-Bayhaqiy na wengineo wameipokea kwa cheni za wapokezi Swahiyh kutoka kwa Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam…”
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 173
- Imechapishwa: 19/01/2026
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
59 – Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam (150-224)[1]
219 – ad-Daaraqutwniy amesema: Muhammad bin Makhlad ametuhadithia: al-´Abbaas bin Muhammad ad-Duuriy ametuhadithia: Nimemsikia Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam akisema juu ya Hadiyth zinazozungumzia kuhusu Kuonekana, Mahali pa kuwekea miguu, Mola wetu anacheka kwa kukata tamaa waja Wake licha ya mabadiliko Yake ya hali zao yako karibu, Mola wetu alikuwepo kabla ya kuumba mbingu, Moto hautojaa mpaka pale atakapoweka Mola wako (´Azza wa Jall) mguu Wake ambapo utasema: “Tosha, tosha” na Hadiyth nyenginezo mfano wa hizo:
“Hadiyth hizi ni Swahiyh. Wamezipokea waaminifu baadhi kutoka kwa wengine mpaka zikatufikia. Tunaona kuwa ni za haki. Lakini tunapoulizwa ni anaweka mguu Wake namna gani au anacheka namna gani, tunasema kuwa hatuzifasiri na hatujamsikia yeyote akizifasiri.”[2]
Abu ´Ubayd ni mmoja katika wale vigogo wa Ijtihaad na bingwa wa lugha. Inakutosha kwamba Abu Ishaaq bin Raahuuyah amesema:
“Allaah anapenda uadilifu. Abu ´Ubayd ni mjuzi zaidi kuliko mimi, ash-Shaafi’iy na Ahmad.”
Abu ´Ubayd alifariki mwaka 224. Aliandika kitabu ”Ghariyb-ul-Hadiyth” lakini hakujishughulisha kufasiri khabari za sifa. Aliona kwamba hapakuwa na tafsiri kwa mambo hayo isipokuwa kwa mujibu wa muktadha wa kiarabu cha Qur-aan – na Allaah (Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.
[1] Mtunzi wa kitabu amesema katika ufupisho wake “yeye na ash-Shaafi´iy wamezaliwa mnamo 150”.
[2] Mtunzi amepokea masimulizi haya kupitia kwa ad-Daraaqutwniy. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh, kama alivotaja mtunzi wa kitabu katika ufupisho wake. Ibn Mandah ameipokea katika “at-Tawhiyd” (2/96 – mswada) kupitia njia zingine, kutoka kwa ad-Duuriy. Ibn Taymiyyah amesema katika “al-Hamawiyyah”:
”al-Bayhaqiy na wengineo wameipokea kwa cheni za wapokezi Swahiyh kutoka kwa Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam…”
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 173
Imechapishwa: 19/01/2026
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/153-hatujui-namna-gani/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket