Ama kupelekea jambo la amri na katazo kwenye unyoofu wa kupindukia, basi mfano wake ni kama mtu anayetawadha huku akiwa na wasiwasi kupita kiasi hadi wakati wa swalah unapita, akakariri Takbiyrat-ul-Ihraam kiasi cha kumkosesha kusoma al-Faatihah pamoja na imamu au kukaribia kuikosa Rak´ah au akajitia ushupavu wa kutenda kwa wema uliozidi mpaka kiasi cha kutokula chochote kutoka kwa watu wa kawaida wa waislamu kwa khofu ya kuingiliwa na mambo ya kutia shaka. Kwa yakini uchamungu ulioharibika umewapata baadhi ya wafanya ´ibaadah ambao wamepungua fungu lao katika elimu mpaka akawa anakataa kula chochote kutoka katika ardhi za Kiislamu na alikuwa akijilisha kwa kile kinacholetwa kwake kutoka ardhi za manaswara na alikuwa akituma kwa makusudi ili kupata hilo. Hivyo ujinga mwingi na uchupaji mipaka ukamtia katika kuwadhania vibaya waislamu na kuwa na dhana njema kwa manaswara. Tunajikinga kwa Allaah kutokana na kukoseshwa nusura!
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 28-29
- Imechapishwa: 03/08/2025
Ama kupelekea jambo la amri na katazo kwenye unyoofu wa kupindukia, basi mfano wake ni kama mtu anayetawadha huku akiwa na wasiwasi kupita kiasi hadi wakati wa swalah unapita, akakariri Takbiyrat-ul-Ihraam kiasi cha kumkosesha kusoma al-Faatihah pamoja na imamu au kukaribia kuikosa Rak´ah au akajitia ushupavu wa kutenda kwa wema uliozidi mpaka kiasi cha kutokula chochote kutoka kwa watu wa kawaida wa waislamu kwa khofu ya kuingiliwa na mambo ya kutia shaka. Kwa yakini uchamungu ulioharibika umewapata baadhi ya wafanya ´ibaadah ambao wamepungua fungu lao katika elimu mpaka akawa anakataa kula chochote kutoka katika ardhi za Kiislamu na alikuwa akijilisha kwa kile kinacholetwa kwake kutoka ardhi za manaswara na alikuwa akituma kwa makusudi ili kupata hilo. Hivyo ujinga mwingi na uchupaji mipaka ukamtia katika kuwadhania vibaya waislamu na kuwa na dhana njema kwa manaswara. Tunajikinga kwa Allaah kutokana na kukoseshwa nusura!
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 28-29
Imechapishwa: 03/08/2025
https://firqatunnajia.com/15-ujinga-uliopitiliza/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket