15. Hadiyth ”Mtume wa Allaah hakuwahi kuvua viatu vyake… ”

al-Haakim (1/139) amesema: Muhammad bin Swaalih na Ibraahiym bin ´Iswmah ametuhadithia: as-Sarriy bin Khuzaymah ametuhadithia: Muusa bin Ismaa´iyl ametuhadithia … Vilevile Abul-Waliyd al-Faqiyh ametufahamisha: al-Hasan bin Sufyaan ametuhadithia: Ibraahiym bin al-Hajjaaj ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Muthannaa al-Answaariy ametuhadithia, kutoka kwa Thumaamah, kutoka kwa Anas, ambaye ameeleza:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwahi kuvua viatu vyake wakati wa swalah isipokuwa mara moja tu, ambapo alivua na watu nao wakavua. Akasema: ”Mna nini nyinyi?” Wakasema: ”Umevua nasi tukavua.” Akasema: ”Jibriyl amekuja na kunijulisha kuwa vina uchafu.”

al-Haakim amesema:

”Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy. Amesimulia kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Muthannaa kwa lengo la kumjengea hoja. Si al-Bukhaariy wala Muslim hakuna aliyeikpokea.”

adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

Haafidhw al-Haythamiy amesema:

“Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw”. Wanaume wake ni wanaume Swahiyh. al-Bazzaar ameipokea kwa toleo fupi.”[1]

[1] Majma´-uz-Zawaa’id (2/56).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 03/06/2025