al-´Ayyaashiy amesema:
“Jaabir amesema: “Nilimuuliza Abu Ja´far: “Ni lini kiongozi wa waumini alipewa jina hilo?” Akasema: “Ninaapa kwa Allaah kwamba Aayah isemayo:
وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ
“Pindi Mola wako alipowaleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao [na akawauliza]: “Je, Mimi siye Mola wenu?”[1]
imeteremshwa namna hii:
وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَى أَنفُسِهِمْ أَلَسْتَ بِرَبِّكُمْ و أن محمدا رسول الله نبيكم و أن عليا أمير المؤمنين
“Pindi Mola wako alipowaleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao [na akawauliza]: “Je, Mimi siye Mola wenu, kwamba Muhammad Mtume wa Allaah Nabii wenu na kwamba ´Aliy kiongozi wa waumini?”
Allaah akampa jina hilo la kiongozi wa waumini.”
Jaabir amesema: “Abu Ja´far alinambia: “Ee Jaabir! Lau wajinga wangelijua ni lini ´Aliy alipewa jina “Kiongozi wa waumini” basi wasingelimpora haki yake.” Nikasema: “Ni lini aliitwa hivo?” Akasema: “Ni pale Aliposema:

Jaabir! Ninaapa kwa Allaah kwamba namna hii ndivo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuja nayo.”
Allaah amemtakasa Abu Ja´far kutokamana na uongo huu wa wazi kumzulia Allaah na Kitabu Chake ambao unajulikana mpaka na wale wasiokuwa wasomi. Hata Jaabir pamoja na uongo wake hawezi kuthubutu kusema uongo namna hii. Uongo kama huu unatoka kwa Baatwiniyyah kama al-´Ayyaashiy na mfano wake.
Wahalifu wameongeza katika Aayah:
و أن محمدا رسول الله نبيكم و أن عليا أمير المؤمنين
“… kwamba Muhammad Mtume wa Allaah Nabii wenu na kwamba ´Aliy kiongozi wa waumini?”
Nyongeza kuhusu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni sitara na udanganyifu. Malengo ni kwamba na mimi ni kiongozi wa waumini. Wako wapi Mitume na Manabii wengine? Ni kwa nini Allaah hakuchukua fungamano kutoka kwa wanaadamu kwamba wao ni Mitume na Manabii wa Allaah? Kwa nini achukue ahadi kwao tu juu ya kwamba waamini kuwa ´Aliy ndiye kiongozi wa waumini? Jawabu kwa mujibu wa Baatwiniyyah ni kwa sababu yeye ni bora kuliko Manabii na Mitume. Shani ya mambo ni uongo tu na ukafiri wenye kupandiana. Wameharibu maana ya Aayah inayothibitisha Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ili tu waweze kutakasa msingi wa uongo wao, makanusho yao na uadui wao dhidi ya Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Aayah hizi zimeteremshwa Makkah. Qur-aan ilisomwa na wanaume, wanawake, waungwana, watumwa na watoto kipindi ambacho Mtume wa Allah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa hai. Je, hivi wote walikubaliana juu ya kufutwa kwa misitari:

Ni kwa nini basi ´Aliy hakuirudisha mahala pake stahiki? Ni kwa nini hakuyasema hadharani yale yaliyofutwa? Kwani yeye si ndiye alikuwa kiongozi wa waumini na jeshi lilikuwa chini yake.
[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/41).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 208-209
- Imechapishwa: 19/09/2018

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 208-209
Imechapishwa: 19/09/2018
https://firqatunnajia.com/147-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-kumi-wa-al-araaf/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)