Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
118 – Hatufarikishi kati ya yeyote katika Mitume Wake. Tunawasadikisha wote kwa yale waliyokuja nayo.
MAELEZO
Tumeshatangulia kuyataja. Ni lazima kuwaamini Mitume wote, kuanzia wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao, wale Mitume waliotajwa na Allaah ndani ya Qur-aan na wale ambao hawakutajwa. Tunawaamini Mitume wote ambao Allaah amewatumiliza kwa waja Wake. Yule anayewaamini baadhi na akawakufuru baadhi ya wengine ni kafiri. Anayemkanusha Mtume mmoja tu anakuwa amewakufuru Mitume wote:
إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ حَقًّا ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا
“Hakika wale waliomkanusha Allaah na Mtume Wake na wanataka kufarikisha baina ya Allaah na Mtume Wake na wanasema: “Tunaamini baadhi na tunawakanusha baadhi”; na wanataka kuchukua njia iliyo baina ya hayo – hao ndio makafiri wa kweli. Na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.””[1]
Mayahudi ni makafiri kwa sababu wamewakufuru Mitume wawili watukufu: ´Iysaa na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam). Manaswara ni makafiri kwa sababu wamekufuru ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wale wanaosema hii leo eti mayahudi, manaswara na waislamu wote ni waumini na wanaita katika umoja wa dini na mazungumzo, ni wapotofu. Fikira yao ni ya makosa na wanachanganya kati ya haki na upotofu, imani na ukafiri. Kwa sababu baada ya kutumilizwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuna dini nyingine ambayo ni sahihi zaidi ya Uislamu:
وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ
”Yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[2]
Uislamu umefuta dini zingine zote zilizokuwa kabla yake na imewaamrisha watu, majini, mayahudi, manaswara, wasiokuwa wasomi, waarabu na wasiokuwa waarabu kumfuata mteuliwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hiyo imani haisihi isipokuwa kwa kumfuata Mtume huyu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1]4:150-151
[2]3:85
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 153-154
- Imechapishwa: 24/11/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 153-154
Imechapishwa: 24/11/2024
https://firqatunnajia.com/144-hatumbagui-mtume-yeyote/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)