Swali 141: Ni ipi hukumu ya ambaye anasafiri kwa ajili ya rambirambi ya jamaa au rafiki? Je, inafaa kutoa mkono wa pole kabla ya kuzikwa[1]?

Jibu: Hatujui ubaya wowote kusafiri kwa ajili ya rambirambi ya jamaa au rafiki. Kufanya hivo kuna kuwaunga, kuwaliwaza na kupunguza maumivu ya msiba. Hapana vibaya kutoa pole kabla na baada ya mazishi. Kila ambavo hayo yatafanyika karibu zaidi na kipindi cha msiba ndivo inakuwa kamili zaidi kupunguza maumvu yake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/376).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 102
  • Imechapishwa: 21/01/2022