Kuitaja kwetu kuwa ni nzuri ni kwenda mbambali na kauli ya baadhi yao, kama ilivyo katika ”at-Tadriyb-ur-Raawiy”, kwamba nzuri ni ile yenye udhaifu wa karibu unaovumilika. Na pia kwa kauli ya al-Baghawiy kwamba yaliyomo katika vitabu vya Sunan ni Hadiyth nzuri. Kauli hizi mbili zina mwelekeo sahihi kwa mtazamo wetu, hata kama tafsiri ya nzuri iliyo mashuhuri ni tofauti na hizo. Imaam an-Nawawiy amesema katika ”at-Taqriyb”:
”Abu Daawuud amepokea katika ”as-Sunan” yake Hadiyth Swahiyh, ile iliyo karibu nayo na inayofanana nayo. Na Hadiyth yenye udhaifu mkali huubainisha. Na ile asiyotaja chochote juu yake basi ni salama. Kwa msingi huu kila tulichokikuta katika kitabu chake bila yeye kukisahihisha mwingine wala kukidhoofisha, basi ni nzuri kwa Abu Daawuud. Kwa sababu kinachofaa kukijengea hoja hakiendi nje ya Swahiyh au nzuri. Bali Ibn Rushd ”Kile ambacho [Abu Daawuud] amekinyamazia huenda kikawa Swahiyh, hata kama si hivyo kwa wengine.”[1]
Baada ya hayo, hakika wapokezi wa Hadiyth ya Thawbaan wote ni wenye kuaminika na wenye kuridhiwa, kama inavyojulikana kwa kurejea majina yao katika vitabu vya tabaka za wapokezi. Tayari umejua jibu la shaka ya kukatika katika cheni yake. Kwa hivyo ikaongezeka nguvu, ikawa nzuri na ikafaa kujengewa hoja – na sifa zote njema ni za Allaah.
[1] Hapana shaka kwa wanaoifahamu elimu hii Tukufu kwamba katika ”as-Sunan” ya Abu Daawuud kuna Hadiyth ambazo cheni zake ni Swahiyh. Lakini kinachopaswa kuchunguzwa ni kile kilichoenea kwa wanazuoni wa baadaye kwamba kila alichokinyamazia Abu Daawuud basi kinafaa kukijengea hoja, kama ilivyotajwa na mwandishi. Basi tambua kwamba kauli ya Abu Daawuud ”… basi ni chenye kufaa” – kama ilivyonukuliwa katika ”at-Tadriyb” – kuna uwezekano akamaanisha kwamba kinafaa kukijengea hoja, na Imaam an-Nawawiy ameonelea maana hiyo. Pia inawezekana akamaanisha kwamba kinafaa kukitumia kama ushahidi kwa sababu si dhaifu sana, maoni yaliyochaguliwa na Kiongozi wa Hadiyth Haafidhw al-´Asqalaaniy. Hii ya pili ndio kauli ninayoiona kuwa sahihi kwa mambo mengi yasiyo na nafasi ya kuyataja sasa. Lakini katika yanayovutia ni pale Abu Daawuud aliposema:
”Na kilicho na udhaifu mkali nimeubainisha.”
Maana yake kwa dhana ni kwamba kile kilicho na udhaifu usio mkali hakubainishi, kwa maana kwamba hukinyamazia. Matokeo yake ni kwamba hili ndilo linalokusudiwa na kauli yake baadaye ”Na kile ambacho sikukutaja chochote juu yake basi ni chenye kufaa”. Basi tafakari, tafuta lililo sahihi na usidanganyike na yaliyoenea miongoni mwa watu.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 26-26
- Imechapishwa: 05/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 26-26
Imechapishwa: 05/04/2026
https://firqatunnajia.com/14-wakati-abu-daawuud-anapoinyamazia-hadiyth/