54 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: Da´laj bin Ahmad ametukhabarisha: Muhammad bin ´Aliy bin Zayd ametukhabarisha: Sa´iyd bin Mansuur ametuhadithia: al-Haarith bin ´Ubayd al-Iyaadiy ametuhadithia: Maalik bin Diynaar ametuhadithia: Abud-Dardaa’ amesema:

”Kikubwa ninachochelea juu ya nafsi yangu ni kuambiwa ´Ulijua, ee ´Uwaymir!`, ambapo nijibu ´Ndio`. Ndipo niambiwe ´Uliyafanyia kazi yale uliyojifunza?`.”

55 – Abu Sa´iyd al-Hasan bin Muhammad bin ´Abdillaah bin Hasnawayh al-Aswbahaaniy ametukhabarisha: Abu Ja´far Ahmad bin Ibraahiym at-Taymiy ametuhadithia: ´Imraan bin ´Abdir-Rahiym ametuhadithia: al-Husayn bin Hafsw ametuhadithia: Nimemsikia Sufyaan akisema: Abud-Dardaa’ amesema:

”Mimi sichelei kuambiwa ´Ni yepi uliyojifunza, ee ´Uwaymir?`; lakini ninachochelea ni kuambiwa ”Uliifanyia nini elimu yako, ee ´Uwaymir?`.”

56 – Muhammad bin Ahmad bin Rizq na al-Hasan bin Abiy Bakr wametukhabarisha: Abu Bakr Ahmad bin Sulaymaan bin Ayyuub al-´Abbaadaaniy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdil-Malik ad-Daqiyqiy ametukhabarisha: ´Ubaydullaah bin Muusa ametuhadithia: Abu Bishr al-Halabiy ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:

“Imani haihusiani na madai wala kutamani; hakika hapana vyengine imani ni kile kilichothibiti moyoni na kikasadikishwa na matendo. Yule mwenye kuzugumza vizuri na asitende basi Allaah humrudishia matendo yake, na yule mwenye kuzungumza vizuri na akatenda mema basi Allaah hukipandisha kitendo chake. Hilo ni kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake pekee linapanda neno zuri na kitendo chema hukiinua juu.”[1]

57 – Abul-Qaasim ´Abdur-Rahmaan bin Ahmad bin Ibraahiym al-Qazwiyniy ametukhabarisha: ´Aliy bin Ibraahiym bin Salamah al-Qattwaan ametukhabarisha: Abu Haatim ar-Raaziy ametuhadithia: Abu ´Umar al-Hawdhwiy ametuhadithia: al-Mubaarak bin Fadhwaalah ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan, aliyesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

وَكُلَّ إِنسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ

“Kila mtu Tumemfungia matendo yake shingoni mwake.”[2]

”Bi maana matendo yake.”

[1] 35:10

[2] 17:13

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 12/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy