´Aaswim bin ´Aliy, mwalimu wake al-Bukhaariy
“Nilijadiliana na Jahm ilidhihirika kutokana na maneno yake ya kwamba haamini kuwa kuna Mola juu ya mbingu.”
Watu 120 000 walikuwa wakihudhuria darsa za ´Aaswim. Ibn Ma´iyn amesema kumuhusu:
”Yeye ndiye bwana wa waislamu.”
ad-Daaraqutwniy amesema: Muhammad bin Makhlad ametuhadithia: al-´Abbaas bin Muhammad ad-Duuriy ametuhadithia: Nimemsikia Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam akisema juu ya Hadiyth zinazozungumzia kuhusu Kuonekana, Mahali pa kuwekea miguu, Mola wetu anacheka kwa kukata tamaa waja Wake licha ya mabadiliko Yake ya hali zao yako karibu, Mola wetu alikuwepo kabla ya kuumba mbingu, Moto hautojaa mpaka pale atakapoweka Mola wako (´Azza wa Jall) mguu Wake ambapo utasema: “Tosha, tosha” na Hadiyth nyenginezo mfano wa hizo:
“Hadiyth hizi ni Swahiyh. Wamezipokea waaminifu baadhi kutoka kwa wengine mpaka zikatufikia. Tunaona kuwa ni za haki. Lakini tunapoulizwa ni anaweka mguu Wake namna gani au anacheka namna gani, tunasema kuwa hatuzifasiri na hatujamsikia yeyote akizifasiri.”[1]
Ishaaq bin Raahuuyah amesema:
“Allaah anapenda uadilifu. Abu ´Ubayd ni mjuzi zaidi kuliko mimi, ash-Shaafi’iy na Ahmad bin Hanbal.”
Ibn Battwah sade: Ibn Makhlad ametuhadithia: ar-Ramaadiy ametuhadithia:
”Nilimuuliza Nu´aym bin Hammaad kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ
”Naye Yu Pamoja nanyi popote mlipo.”[2]
Akasema: “Maana yake ni kwamba hakuna kinachofichika Kwake kwa ujuzi Wake. Je, huoni pale Aliposema:
مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ
”Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao.”[3]?
Anachokusudia ni kwamba hakuna chochote kinachojificha Kwake.”
Nu´aym bin Hammaad amesema tena:
“Yule mwenye kumfananisha Allaah na viumbe Vyake amekufuru. Yule mwenye kupinga yalwe aliyojisifu nayo Mwenyewe amekufuru. Hakuna katika yale aliyojisifu Mwenyewe nayo wala Mtume Wake ufananishaji.”[4]
Haya yamesihi na kuthibiti kutoka kwa Nu´aym bin Hammaad, mwalimu wake al-Bukhaariy, ambaye Imaam Ahmad bin Hanbal amesema juu yake:
”Yeye ni nguzo miongoni mwa nguzo za Sunnah zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Ameyataja Haafidhw as-Sulaymaaniy.
Swaalih bin adh-Dhwurays amesimulia:
”´Abdullaah alimpiga ndugu yake kichwani kiatu, ambaye alikuwa na ´Aqiydah ya Jahm. Nilimuona akimpiga kwa kiatu chake kichwani mwake na akisema: ”Hapana, mpaka useme:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[5]
Kwa maana ya Yeye kuwa mbali na viumbe Wake.”[6]
Ameipokea Ibn Abiy Haatim katika “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”.
Amesema tena:
”Kuna bwana mmoja alifungwa kwa sababu ya kuwa na ´Aqiydha ya Jahmiyyah. Baadaye akatubu. Kisha mtu huyo akaletwa kwake ili ampe mtihani. Hishaam akamwambia: “Je, unashuhudia ya kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake hali ya kutengana mbali na viumbe Vyake?” Mtu huyo akasema: “Sijui nini maana ya kuwa mbali na viumbe Vyake.” Ndipo Hishaam akasema: “Mrudisheni gereza. Bado hajatubu.”
Hishaam bin ´Ubaydillaah alikuwa mmoja wa maimamu wa Fiqh katika madhehebu ya Abu Haniyfah.
[1] Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Taymiyyah katika ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (5/51).
[2] 57:04
[3] 58:7
[4] al-Laalakaa’iy (936).
[5] 20:05
[6] Cheni yake ya wapokezi haina neno kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mukhtaswar-ul-´Uluww” (193).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 60-63
- Imechapishwa: 23/12/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 60-63
Imechapishwa: 23/12/2025
https://firqatunnajia.com/14-mpaka-useme-ametengana-mbali-na-viumbe-wake/