696- Aws bin Aws ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Siku yenu bora ni ijumaa. Ndani yake ndio kaumbwa Aadam, ndio kafa, ndipo kutakuwa parapanda na ndio kutakuwa kufa. Hivyo basi kithirisheni kuniswali, kwani hakika swalah zenu zinaonyeshwa kwangu.” Wakasema: “Wakasema: “Ni vipi unaonyeshwa swalah zetu ilihali umeshaoza?” Akasema: “Hakika Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameuharamishia udongo kula viwiliwili vyetu.”

Ameipoke Abu Daawuud, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” na matamshi ni yake na ni timilifu zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/436)
  • Imechapishwa: 28/04/2017