Mambo si kama wanavosema Hanafiyyah, kwamba imani ni kutamka kwa ulimi na kukubali kwa moyo peke yake.

Sio kama wanavosema Karraamiyyah, kwamba imani ni kutamka kwa ulimi peke yake.

Sio kama wanavosema Ashaa´irah, kwamba imani ni kuamini moyoni peke yake.

Sio kama wanavosema Jahmiyyah, kwamba imani ni kutambua kwa moyo peke yake.

Murji-ah wako makundi manne. Kundi baya zaidi ni Jahmiyyah. Kwa mujibu wa ´Aqiydah yao Fir´awn anakuwa ni muumini, kwa sababu alikuwa mtambuzi. Vilevile Ibliys anakuwa ni muumini, kwa sababu alikuwa mtambuzi.

Kwa mujibu wa maoni ya Ashaa´irah, ambao wanaona kuwa imani ni kusadikisha moyoni peke yake, Abu Lahab, Abu Twaalib, Abu Jahl na washirikina wengine wanakuwa ni waumini, kwa sababu wanayakinisha kwa mioyo yao. Wanamsadikisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya mioyo yao, lakini kiburi na hasadi ndivyo vilivyowafanya kutomfuata. Mayahudi ndani ya mioyo yao wanatambua kuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakinikilichowazuia kumfuata ni hasadi na kiburi:

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ

“Wale Tuliowapa Kitabu wanamjua kama wanavyowajua watoto wao.”[1]

قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَفَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ

“Hakika tunajua kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha alama za Allaah. Hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha alama za Allaah.”[2]

Hawakukadhibisha maana yake ni kwamba wanakusadikisha. Abu Twaalib alisema:

Nilijua kuwa dini ya Muhammad ni dini ya haki

na ndio dini bora kabisa ya kiumbe

na kama isingelikuwa kuogopa lawama au kutukanwa

basi mgeniona ni mwenye kuikubali waziwazi kabisa[3]

[1]2:146

[2]6:33

[3]al-Bidaayah wan-Nihaayah (3/42).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 146-147
  • Imechapishwa: 19/11/2024