Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
107 – Tunawaombea msamaha wale wafanya makosa katika wao, tunachelea juu yao na wala hatuwakatii tamaa.
MAELEZO
Tunawaombea msamaha watenda dhambi, kwa sababu ni ndugu zetu. Tunawaombea kwa Allaah awasamehe na awaongoze. Hii ni haki ya imani juu yetu:
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ
“Basi jua kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na omba msamaha kwa dhambi zako na za waumini wa kiume na waumini wa kike.”[1]
Hatumkatishi tamaa mtenda dhambi kutokana na rehema za Allaah, kama wanavofanya Khawaarij na Mu´tazilah. Mtenda dhambi yuko katika khatari ya kuadhibiwa na Allaah ndiye mwenye kuamua kama atamsamehe au kumuadhibu, lakini akitubu basi Allaah anamsamehe:
إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ
“Hakika hawakati tamaa na faraja ya Allaah isipokuwa watu makafiri.”[2]
وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ
“Na nani anayekata tamaa na rehema za Mola wake isipokuwa waliopotea.”[3]
قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعاً إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
“Sema: “Enyi waja Wangu ambao mmepindukia juu ya nasfi zenu: “Msikate tamaa na rehema za Allaah. Kwani hakika anasamehe madhambi yote. Kwani hakika Yeye ni mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[4]
Wa´iydiyyah, wakiongozwa na Khawaarij na vifaranga vyao, ndio ambao huwakatisha watu tamaa na rehema za Allaah na kuwatoa nje ya dini kutokana na dhambi zao, ijapokuwa dhambi hizo ni chini ya shirki.
[1]47:19
[2]12:87
[3]15:56
[4]39:53
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 141
- Imechapishwa: 17/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)