Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ummah huu umefaradhishiwa kufanya Hijrah kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu na itaendelea kubaki mpaka Qiyaamah kitaposimama. 

MAELEZO

Kuhama kumeambatanishwa na kufanya jihaad katika njia ya Allaah. Isitoshe ni faradhi iliobaki na ambayo haikufutwa. Ni lazima kwa kila muislamu anayehitaji kuhajiri afanye hivo. Haijuzu kwa muislamu kuishi katika mji wa kikafiri ilihali hawezi kuidhihirisha dini yake. Katika hali hiyo itakuwa ni lazima kuhama kwenda katika mji wa waislamu. Kwa hiyo ni faradhi yenye kubaki. Hayo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hijrah haitosimama mpaka Tawbah isimamishwe. Na Tawbah haitosimamishwa mpaka jua lichomoze kutoka magharibi.”[1]

[1] Abu Daawuud (3479), Ahmad (28/111) (16906).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 266-267
  • Imechapishwa: 10/02/2021