86 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Ibraahiym bin al-Ash´ath ametuhadithia: ´Abdullaah bin Maymuun al-Qaddaah ametuhadithia, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Umayyah, ambaye ameeleza:
“Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) alimwambia Muusa (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam): ”Hakika Mimi nakubali swalah ya anayenyenyekea kwa utukufu Wangu na asiyejikweza juu ya viumbe Wangu; akalazimisha moyo wake kuniogopa, akautumia mchana kwa kunitaja, akaizuia nafsi yake na matamanio kwa ajili Yangu, akamlisha mwenye njaa, akamvisha asiye na nguo na akamuhifadhi mgeni. Basi huyo ndiye ambaye uso wake utang’aa siku ya Qiyaamah kama jua. Huniomba, Namuitikia. Naniomba, Nampa. Nampa busara katika ujinga na nuru katika giza. Namlinda kwa utukufu Wangu na Nawafanya Malaika Wangu wamchunge. Mfano wa mja huyo miongoni mwa watu ni mfano wa Bustani za ´Adn ndani ya Bustani nyingine – matunda yake hayakatiki, wala hali yake haibadiliki.'”
87 – Muhammad bin Yahyaa bin Abiy Haatim ametuhadithia: Ja´far bin an-Nu´maan ar-Raaziy ametuhadithia, kutoka kwa Yuusuf bin Asbaatw, ambaye amesema:
“Inatosha kiasi kidogo cha uchaji kuliko matendo mengi. Inatosha kiasi kidogo cha unyenyekevu kuliko jitihada nyingi.”
88 – Muhammad bin ´Aliy ametuhadithia: Ibraahiym bin al-Ash´ath ametuhadithia:
”Nilimuuliza al-Fudhwayl kuhusu kujinyenyekeza, akasema: “Kujinyenyekeza ni kuinyenyekea haki na kujisalimisha nayo. Hata kama utasikia kutoka kwa mtoto mdogo unaikubali kutoka kwake. Hata kama utaisikia kutoka kwa mjinga kabisa miongoni mwa watu unaikubali kutoka kwake.”
89 – Muhammad bin Haaruun amenihadithia: Abu Swaalih al-Farraa’ amenihadithia: Nimemsikia Ibn-ul-Mubaarak akisema:
“Kilele cha unyenyekevu ni ni kuishusha nafsi yako mbele ya yule aliye chini yako katika neema za dunia ili umwonyeshe kuwa huna ubora juu yake kwa sababu ya dunia, na kuinua nafsi yako juu ya yule aliye juu yako katika neema za dunia ili umwonyeshe kuwa hana ubora juu yako kwa sababu ya dunia yake.”
90 – Abu Muhammad Naswr bin Tarkhaan al-Balkhiy ametuhadithia: ´Umar bin Khaalid ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah, ambaye amesema:
“Yeyote aliyekirimiwa mali, uzuri, nguo au elimu kisha asinyenyeke, basi hiyo itakuwa ni maangamizi kwake siku ya Qiyaamah.”
91 – Muhammad bin ´Uthmaan al-´Ijliy ametuhadithia: Abu Usaamah ametuhadithia, kutoka kwa Juwaybir, kutoka kwa adh-Dhwahhaak, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ
”Wabashirie wanyenyekevu.”[1]
”Kwa maana wale wenye kujinyeneyekeza.”
92 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Dhakwaan amenihadithia:
”an-Najaashiy alipata ugeni baada ya kupata neema. Akawa amevaa mavazi mazito ya kifakhari na ameacha kichwa chake kikiwa wazi. Baadhi ya watu wakasema: “Ee mfalme, si ulisema umetunukiwa na umefurahi?” Akasema: “Ndiyo.” Wakauliza: “Mbona basi unyenyekevu huu?” Akasema: “Nimesoma miongoni mwa yale Allaah aliyomteremshia ´Iysaa bin Maryam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Nikikupa neema, basi ikubali kwa unyenyekevu ili nikamilishe juu yako.”
[1] 22:34
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 116-122
- Imechapishwa: 03/02/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 116-122
Imechapishwa: 03/02/2026
https://firqatunnajia.com/13-unyenyekevu-ni-kitu-gani/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket