Allaah (Ta’ala) amewawekea katika Shari´ah waja wake aina mbalimbali ya ´ibaadah zinazoonyesha unyenyekevu wa viungo vya mwili unaotokana na kunyenyekea kwa moyo, kudhalilika kwake na kujivunjavunja kwake. Miongoni mwa ´ibaadah kubwa ambayo inadhihirisha viungo vya mwili kumnyenyekea Allaah ni swalah. Allaah (Ta´ala) amewasifu waswaliji wanyenyekevu na akasema:
قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ
“Hakika wamefaulu waumini; ambao katika swalah zao ni wenye kunyenyekea.”[1]
Kumeshatangulia jinsi baadhi ya Salaf walivyofasiri unyenyekevu ndani ya swalah. Ibn Lahiy’ah amepokea kutoka kwa ‘Atwaa’ bin Yasaar (Rahimahu Allaah) kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr (Rahimahu Allaah), ambaye amesema:
“Wamenyenyekea sana kiasi cha kwamba hawamjui ni nani aliye upande wao wa kulia wala upande wao wa kushoto. Hawageuki kutoka kwenye ule unyenyekevu unaomstahikia Allaah ( ́Azza wa Jall).”
Ibn-ul-Mubaarak amepokea kutoka kwa Abu Ja´far, kutoka kwa Abu Layth, kutoka kwa Mujaahid, ambaye amesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):
وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ
”… simameni mbele ya Allaah hali ya kuwa ni wanyenyekevu.”[2]
“Unyenyekevu ni kule kunyenyekea, kutojikweza, kutazama chini na kutulizana – rehema kutoka kwa Allaah (Ta’ala). Pindi mmoja katika wanazuoni anaposimama kuswali, basi anamtukuza Mwingi wa rehema kiasi cha kwamba hatazami huku na huku, kugeuka nyuma, kugeuza kokoto, kucheza na chochote au kuizungumzisha nafsi yake kitu chochote katika dunia labda iwe kwa usahaulifu.”
Mansuur amesimulia kutoka kwa Mujaahid (Rahimahu Allaah) ambaye amesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ
“Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhilah na radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu.”[3]
“Kwa maana ya unyenyekevu wakati wa kuswali.”
al-Fadhwl bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
”Swalah ni mbili mbili. Unakaa Tashahhud baada ya kila Rak´ah mbili, nyenyekea, unajidhalilisha, unatulia, unyanyue mikono yako kwa Mola wako (´Azza wa Jall) kwa kuomba na kusema: “Ee Mola! Ee Mola! Ee Mola!” Ambaye hakufanya hivo ni upungufu.”[4]
Ameipokea Imaam Ahmad, an-Nasaa’iy na at-Tirmidhiy.
´Uthman (Radhiya Allaahu ‘anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
”Hakuna muislamu yeyote anayeswali swalah ya faradhi na akafanya vizuri wudhuu´, unyenyekevu na Rukuu´ yake, isipokuwa inakuwa ni kafara kwa yale madhambi yalioko kabla yake, muda wa kuwa hajafanya madhambi makubwa. Inakuwa hivo mwaka mzima.”[5]
Ameipokea Muslim.
[1] 23:01-02
[2] 02:238
[3]48:29
[4] Ahmad (1/211), Abu Daawuud (1296) na at-Tirmidhiy (385). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (385).
[5] Muslim (228).
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 60-64
- Imechapishwa: 24/11/2025

Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 60-64
Imechapishwa: 24/11/2025
https://firqatunnajia.com/13-unyenyekevu-ndani-ya-swalah/