Miongoni mwa mambo muhimu kwa mwenye kuhiji ni kutukuza na kuheshimu alama za Allaah, kutambua utukufu wa maeneo matukufu, kwa namna ya kwamba atekeleze ´ibaadah ya Hajj kwa unyenyekevu, heshima, mapenzi na utiifu kwa Allaah, Mola wa walimwengu. Alama ya hili ni kutekeleza ´ibaadah ya Hajj kwa utulivu na adabu, bila kufanya haraka wala jazba, jambo ambalo watu wengi hawalizingatii siku hizi. Ajizoeshe nafsi yake kuwa na subira katika utiifu kwa Allaah, kwani hilo linapelekea kukubaliwa kwa matendo na kupewa ujira mkubwa zaidi.
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewahimiza waja Wake kutukuza nembo Zake na kuzilinda. Amesema (Ta´ala):
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ
“Ndio hivyo iwe na yeyote anayetukuza vitukufu vya Allaah, basi hivyo ni kheri kwake mbele ya Mola wake.”[1]
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ
“Ndivyo hivyo na yeyote anayeadhimisha ´ibaadah za Allaah, basi hayo ni katika uchaji wa nyoyo.”[2]
Makusudio ya matukufu ya Allaah (حرمات الله) ni kila chenye utukufu na ikaamrishwa kukiheshimu ikiwa ni pamoja na ´ibaadah na mengineyo. Aidha ´ibaadah zote za Hajj, Haram na Ihraam.
Nembo za Allaah (شعائر الله) ni alama za dini zilizo dhahiri kukiwemo ´ibaadah zote za Hajj. Amesema (Ta´ala):
إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَآئِرِ اللّهِ
“Hakika vilima vya Swafaa na Marwah ni katika alama za Allaah.”[3]
Kwa hivyo, ee ndugu muislamu, tafakari hayo. Kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amefanya kutukuza alama Zake kuwa ni nguzo ya uchaji na sharti ya ´ibaadah. Aidha amefanya kutukuza matukufu Yake kuwa ni njia ya mja kupata ujira mkubwa na zawadi Yake kuu. Anayetafakari Hajj ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa macho ya mwanafunzi anayetaka kufuata, basi ataona ndani yake picha bora kabisa za kutukuza alama za Allaah katika maneno na vitendo vyake vyote (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[4].
[1] 22:30
[2] 22:32
[3] 02:158
[4] Tazama ”Ahwaal-an-Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) fiyl-Hajj” cha mtunzi Fayswal bin ´Aliy al-Ba´daaniy.
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 19-20
- Imechapishwa: 11/05/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 19-20
Imechapishwa: 11/05/2025
https://firqatunnajia.com/13-kutukuza-na-kuheshimu-nembo-za-allaah/