4 – Hoja tata ya nne wamesema kuwa Shaykh anawapiga vita watu wenye kusema “Laa ilaaha illa Allaah”, wanaswali, wanatoa zakaah, wanafunga, wanahiji na wanamwabudu Allaah.
Jibu ni kwamba watu hawa wamesema “Laa ilaaha illa Allaah”, wanaswali na kadhalika, lakini hata hivyo wamechengua “Laa ilaaha illa Allaah” na wamezibatilisha swalah na ´ibaadah zao kwa kufanya shirki kubwa ambayo ni kumuabudu asiyekuwa Allaah ikiwa ni pamoja na kuwaomba wafu, kuwachinjia, kuwawekea nadhiri na kutufu kwenye makaburi. Neno “Laa ilaaha illa Allaah” maana yake ni kwamba hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Watu hawa wameabudu wengine pamoja na Allaah na hivyo shahaadah haikuwafaa kitu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kusema ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` na akakufuru vile vyenye kuabudiwa badala ya Allaah, basi imeharamika kumwagwa damu na mali yake na hesabu yake iko kwa Allaah (´Azza wa Jall).”[1]
Watu hawa hawakukufuru vile vyenye kuabudiwa badala ya Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:
لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“Hapana kulazimisha katika dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaaghuut [miungu ya uongo] na akamwamini Allaah, kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika.” (02:256)
Ametanguliza kukufuru Twaaghuut kabla ya kumuamini Allaah. Yule mwenye kumuabudu asiyekuwa Allaah hakukufuru Twaaghuut. Maana ya “Laa ilaaha illa Allaah” ni kwamba hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Ndani yake mna makanusho na uthibitishaji. Kukanusha ´ibaadah anazofanyiwa asiyekuwa Allaah na badala yake kuzithibitisha kwa Allaah. Kwa msemo mwingine kubatilisha ´ibaadah za vinavyoabudiwa vyote ikiwa ni pamoja na makaburi, masanamu, mawe, miti, majini, watu, Malaika, Manabii na Mitume na badala yake kuthibitisha ´ibaadah afanyiwe Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirika. Amesema (Ta´ala):
وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ
“Hakika umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka yataporomoka matendo yako na hakika utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” (39:65)
Mwenye kumshirikisha Allaah shirki kubwa matendo yake yote yanabatilika ikiwa ni pamoja na swalah na mengineyo. Vilevile inakuwa ni halali kumwagwa damu yake na kuporwa mali yake, jambo ambalo liko wazi ndani ya Qur-aan, Sunnah na katika uongofu wa makhaliyfah waongofu ambao waliwapiga vita watu wa Yamaamah pamoja na kuwa wanashuhudia ya kwamba hapana mungu mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume Wake. Hata hivyo walisema kuwa Musaylamah ni Nabii. Ikiwa yule mwenye kumsadikisha anayedai utume anakufurishwa na kupigwa vita, vipi asikufurishwe na kupigwa vita mwenye kudai Allaah kuwa na mshirika katika ´ibaadah Zake?
Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, jamaa zake na Maswahabah zake.
[1] Muslim (23).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 58-62
- Imechapishwa: 08/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 58-62
Imechapishwa: 08/02/2026
https://firqatunnajia.com/13-ibn-abdil-wahhaab-anawapiga-vita-wenye-kutamka-shahaadah/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket