Zaidi ya hayo kukatika pekee si kasoro yenye kuharibu, kwani katika Swahiyh Muslim kuna Hadiyth kadhaa zilizokatika, ingawa muunganiko wake umebainika kwa njia nyingine. Kwa sababu aliyekatika lakini mpokezi wake ni mwaminifu si kama mwingine. Ndiyo maana walikubali baadhi ya Hadiyth ambazo katika cheni yake kuna Swahabah anayekosekana kama zimesimuliwa kutoka kwa wasimulizi wenye kuaminika, kama ilivyothibiti katika nafasi yake[1].

[1] Baada ya wewe kujua usahihi wa cheni ya wapokezi ya Hadiyth na kuungana kwake, basi sioni faida ya kupanua mjadala wa uwezekano wa mbali katika kuitetea. Kwa sababu lililokubaliwa katika elimu ya istilahi ni kwamba Hadiyth iliyokatika ni katika aina za Hadiyth dhaifu, kwa sababu ya kutokujulikana kwa mpokezi aliyekosekana. Aidha simjui yeyote katika waandishi wa elimu ya istilahi aliyetamka waziwazi kukubaliwa kwa Hadiyth iliyosimuliwa na wasimulizi wenye kuaminika na ambayo kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi wake kwa namna hii kwa ujumla. Bali katika hilo kuna makinzano mashuhuri yanayotajwa mahali pake. Alichokitaja kuhusu Hadiyth zilizokatika katika Swahiyh Muslim hakiondoi dosari iliyotajwa, maadamu imebainika kuungana kwake kwa njia nyingine. Ama la sivyo lau isingebainika hivyo, basi dosari ingetimia. Basi tafakari hilo!

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 26
  • Imechapishwa: 05/04/2026