Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

99 – Hatuingii katika maneno ya kipuuzi kuhusu Allaah na wala hatuvutani kuhusu dini ya Allaah.

MAELEZO

Hatumpelelezi Allaah. Bali tunamuamini, sifa na majina Yake. Hatuzipindishi wala kuzigeuza maana yake ya dhahiri na tukaleta maana nyingine ambayo haikukusudiwa na Allaah wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa kufuata matamanio yetu na akili zetu pungufu. Huku ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall).

Vilevile hatuvutani kuhusu dini ya Allaah. Hatujadili. Tunamwamini kwa mujibu wa dalili. Yale yaliyothibiti katika Qur-aan na Sunnah hakuna nafasi ya kuyapeleleza. Bali tunayaamini na kujisalimisha nayo, ijapo akili yetu haiyafahamu yote. Kwani akili yetu ni pungufu, vinginevyo tusingemuhitaji Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Mitume. Ikafahamisha kuwa akili ni pungufu na kwamba ni lazima kutumilizwa Mitume ili kuisimamisha haki na kuitokomeza batili.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 134
  • Imechapishwa: 13/11/2024