117 – Hata hivyo haijuzu kwa wanawake kuyatembelea makaburi kwa wingi na kwenda huko mara kwa mara, kwa sababu hilo linaweza kuwapelekea kwenda kinyume na Shari´ah, kama vile kupiga mayowe, kuonyesha mapambo, kuyafanya makaburi kuwa sehemu za mapumziko na kupoteza muda kwa maneno yasiyo na faida, kama inavyoonekana leo katika baadhi ya nchi za Kiislamu. Hayo ndio makusudio ya Hadiyth inayotambulika:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani… ”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”… Allaah amewalaani] wanawake wanaoyatembelea makaburi mara kwa mara.”
Hadiyth hii imepokelewa kutoka kwa Maswahabah kadhaa akiwemo Abu Hurayrah, Hassaan bin Thaabit na ´Abdullaah bin ´Abbaas.
1 – Ama Hadiyth ya Abu Hurayrah ni kutoka njia ya ´Umar bin Abiy Salamah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwake. Ameipokea at-Tirmidhiy (2/156 – Tuhfah), Ibn Maajah (1/478), Ibn Hibbaan (789), al-Bayhaqiy (4/78), at-Twayaalisiy (1/171 – kwa mpangilio wake) na Ahmad (2/337). Tamko jengine ni la at-Twayaalisiy na al-Bayhaqiy. at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”
Baadhi ya wanazuoni wameona kuwa hii ilikuwa kabla ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaruhusu kuyatembelea makaburi. Baada ya kuruhusu wanaume na wanawake walijumuishwa katika ruhusa hiyo. Kuna wengine waliosema kwamba wanawake wamechukizwa kuyatembelea makaburi kutokana na uchache wa subira yao na wingi wa mahuzuniko yao.”
Wanaume wa cheni ya Hadiyth wote ni wenye kuaminika, isipokuwa inapokuja kwa ´Umar bin Abiy Salamah kuna dosari. Hata hivyo Hadiyth yake haishuki chini ya kiwango cha kuwa nzuri. Lakini Hadiyth hii ni Swahiyh kutokana na Hadiyth nyengine ambazo zinaitia nguvu.
2 – Ama Hadiyth ya Hassaan bin Thaabit, ni kutoka njia ya ´Abdur-Rahmaan bin Bahmaan, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Thaabit, kutoka kwa baba yake.
Ameipokea Ibn Abiy Shaybah (4/141), Ibn Maajah (1/478), al-Haakim (1/374), al-Bayhaqiy na Ahmad (2/243), al-Buuswayriy amesema katika ”az-Zawaa-id”, uk. (98/2):
”Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na wanaume wake ni waaminifu.”
Hivo ndivo alivosema, lakini Ibn Bahmaan huyu hakufanywa kuwa mwaminifu isipokuwa na Ibn Hibbaan na al-´Ajliy, ambao wanajulikana kuchukulia wepesi kuwafanya wasimulizi kuwa ni wenye kuaminika. Ibn al-Madiyniy amesema juu yake: ”Hamtambui.” Ndiyo maana Haafidhw amesema katika ”at-Taqriyb”: ”Ni mwenye kukubaliwa.” Kwa maana ya kwamba ikiwa ataungwa mkono. Sikuona mwenye kumfuatilia, lakini ushahidi uliotangulia na unaofuata unahesabika kuwa ni wa kumfuatilia. Kwa hivyo Hadiyth ni yenye kukubaliwa.
3 – Ama Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas, imesimuliwa kupitia njia ya Abiy Swaalih, kutoka kwake kwa matamshi ya mwanzo, isipokuwa tu yeye amesema:
”… wanawake wanaoyatembelea makaburi.”
Katika upokezi mwingine:
”… wanaoyatembelea mara kwa mara.”
Ameipokea Ibn Abiy Shaybah (4/140) na watunzi wanne wa Sunan, Ibn Hibbaan (788), al-Haakim, al-Bayhaqiy, at-Twayaalisiy na upokezi mwingine ni kutoka kwa wawili hao na Ahmad (nr. 2030, 2603, 2986, 3118). at-Tirmidhiy amesema: ”Hadiyth ni nzuri. Abu Swaalih huyu ni mtumwa wa Umm Haaniy bint Abiy Twaalib, jina lake ni Baadhaan. Inasemekana vilevile kwamba anaitwa Baadhaam.”
Yeye ni dhaifu, bali wengine walimshutumu. Hadiyth nimeitaja katika ”as-Silsilah Ahaadiyth-is-Swahiyhah” kwa ziada aliyopwekeka nayo. Nimetaja baadhi ya maono ya maimamu kuhusu hali yake, kwa hivyo mtu arejee huko (223).
Imedhihirika kutokana na uchambuzi wa Hadiyth kwamba lililohifadhiwa ni kwa tamko lisemalo:
”… wanawake wanaoyatembelea mara kwa mara.”
Kwa sababu inaafikiana na Hadiyth ya Abu Hurayrah na Hassaan, vilevile Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas katika mapokezi ya wengi, ingawa kuna udhaifu ndani yake. Kama haifai kuwa ni ushahidi bado haidhuru kitu. Kama haidhuru basi mapokezi mengine kutoka kwa Ibn ‘Abbaas hayadhuru vilevile. Mambo yakishakuwa ni hivo, basi tamko lisemalo:

linafahamisha juu ya kulaaniwa wanawake wanaoyatembelea kwa wingi. Tofauti na wanawake wengine ambao hawahusishwi na laana hiyo. Kwa hivyo haijuzu kuchukua Hadiyth hii na kuipinga kwa Hadiyth zilizotangulia zinazoonyesha kupendekezwa kwa wanawake kuyatembeleaa makaburi, kwa sababu hii ni maalum na zile ni zenye kuenea. Basi kila moja itumike katika mahali pake. Kuoanisha namna hii ni bora zaidi kuliko madai ya kufutwa. Jopo la wanazuoni wameonelea mfano wa haya niliyoyataja. al-Qurtwubiy amesema:
”Laana iliyotajwa katika Hadiyth ni kwa wanawake wanaoyatembelea kwa wingi kwa sababu ya matumizi ya mtindo unaonyesha wingi. Huenda sababu iliyopelekea katika hilo ni kama kupoteza haki ya mume, kujishaua kwa kuonyesha mapambo na mfano wa hayo. Pengine ikasemwa kwamba ikiwa yote hayo yataepukwa, basi hakuna kizuizi kwa kuwaruhusu, kwa sababu kukumbuka mauti kunahitajika na wote wanaume na wanawake.”
ash-Shawkaaniy amesema katika ”Nayl-ul-Awtwaar” (4/95):
”Haya ndiyo maneno yanayopaswa kutegemewa katika kukusanya baina ya Hadiyth za mlango huu ambazo kwa nje zinaonekana kuwa na mgongano.”[1]
[1] as-Swan´aaniy katika ”Subul-us-Salaam” amefanya uoanishaji kama huu, lakini amejengea hoja juu ya kujuzu kwa dalili ambazo ndani yake zinatakiwa kuangaliwa vyema. Kwa hivyo kuzindua jambo hilo:
1 – Hadiyth ya al-Husayn bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa):
“Kwamba Faatwimah bint Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitembelea kaburi la ami yake Hamzah kila ijumaa, kisha akiswali na kulia.”
Ameipokea al-Haakim (1/377), na kutoka kwake al-Bayhaqiy (4/78), ambaye amesema:
”Hadiyth ni yenye kukatika.”
Haafidhw ameinyamazia katika ”at-Talkhiysw” (5/248) na as-Swan´aaniy akamfata. Kunyamaza kwao wawili na kuridhika kwa al-Bayhaqiy kuielezea kuwa imekatika kunaweza kumpa mtu dhana kwamba haina isipokuwa dosari hiyo tu, jambo ambalo sivyo hivyo kama tulivyoelezea karibuni.
2 – Hadiyth ya al-Bayhaqiy katika ”Shu´ab-ul-Iymaan” kwa cheni ya wapokezi ambayo kuna Swahabah anayekosekana:
“Yeyote atakayetembelea kaburi la wazazi wake wawili au mmoja wao kila ijumaa, basi atasamehewa madhambi na kuandikiwa kuwa ni mwenye kuwafanyia wema.”
as-Swan´aaniy naye pia ameinyamazia. Hadiyth hiyo pia ni dhaifu sana, bali ni yenye kubuniwa. Si kwamba kuna Swahabah anayekosekana tu katika cheni yake ya wapokezi, kama alivosema as-Swan´aaniy. Mambo yalivyo ni kwamba imekatika kwa zaidi ya mtu mmoja kwa kuwa ambaye ameirufaisha ni Muhammad bin an-Nu´maan ambaye si mwanafunzi wa Swahabah. al-´Iraaqiy amesema katika ”Takhriyj-ul-Ihyaa´” (4/418) amesema:
”Ameipokea Ibn Abiyd-Dunyaa, nayo kuna zaidi ya msimulizi mmoja anayekosekana katika cheni ya wapokezi. Muhammad bin an-Nu´maan hatambuliki.”
Ameipokea kutoka kwa Yahyaa bin al-´Alaa’ al-Bajaliy kwa cheni yake, kutoka kwa Abiy Hurayrah. Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”as-Swaghiyr” (199). Yahyaa huyu amesemwa kuwa ni muongo na amepingwa na Wakiy´ na Ahmad. Ibn Abiy Haatim (2/209) amesema kutoka kwa Baba yake:
”Hadiyth hii ni dhaifu mno, kana kwamba imetungwa.”
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 235-237
- Imechapishwa: 05/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 235-237
Imechapishwa: 05/08/2026
https://firqatunnajia.com/124-haijuzu-kwa-wanawake-kuyatembelea-makaburi-mara-kwa-mara/