239-
“Atasema:
أَللّهُ أَكْبَرُ
“Allaah ni mkubwa.”
kila ambapo atarusha vijiwe kwenye nguzo tatu. Kisha atasogea mbele ambapo atasimama na akiomba du´aa hali ya kuelekea Qiblah, akinyanyua mikono yake baada ya kiguzo cha kwanza na cha pili. Ama kuhusu kiguzo cha tatu, atarusha na kusema:
أَللّهُ أَكْبَرُ
“Allaah ni mkubwa.”
wakati wa kila kijiwe na kisha aondoke na asisimame mahala hapo.”[1]
[1] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (03/583-584) na (03/584). Tazama tamko lake huko. Pia al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (03/581) na Muslim ameipokea pia.
- Muhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huswn-ul-Muslim
- Imechapishwa: 09/05/2020