Nabii ni yule ambaye amefunuliwa Shari´ah pasi na kuamrishwa kuifikisha. Mtume ni yule ambaye amefunuliwa Shari´ah na pia akaamrishwa kuifikisha. Ni lazima kuwaamini Mitume na Manabii wote. Yule mwenye kuwaamini baadhi yao na akawakufuru wengine, basi amewakufuru wote:
آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللّهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ
”Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola Wake na waumini vilevile; wote wamemuamini Allaah na Malaika Wake na Vitabu vyake na Mitume Yake – hatutafautishi kati ya yeyote katika Mitume Wake na husema: “Tumesikia na tumetii, tunakutaka msamaha Mola Wetu; na marejeo ni Kwako”.”[1]
Miongoni mwa misingi ya imani ni kuamini vitabu ambavyo Allaah amewateremshia navyo Mitume ili kuwaongoza viumbe. Vitabu hivyo vimebeba maneno, wahy na mambo ya Shari´ah ya Allaah (Ta´ala). Amewateremshia MitumeWake ili wawafikishie navyo nyumati zao. Ndani yake mna maamrisho na makatazo na Shari´ah za Allaah (´Azza wa Jall). Baadhi ya vitabu Allaah amevitaja ndani ya Qur-aan na vyengine hakuvitaja. Tunaviamini vitabu vyote, tulivyotajiwa na ambavyo hatukutajiwa. Baadhi yavyo ni Tawraat ambacho amekiteremsha kwa Muusa, Injiyl ambacho amekiteremsha kwa ´Iysaa, Qur-aan ambacho amekiteremsha kwa Muhammad na Zabuur ambacho amekiteremsha kwa Daawuud (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam):
وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا
“… na tumempa Daawuud Zabuur.”[2]
Na sahifa za Ibraahiym (´alayhis-Salaam). Tunaviamini vyote na tunaona kuwa ni kutokana na manufaa ya viumbe, kuwaongoza viumbe na kuwasimamishia hoja. Mwenye kuamini baadhi ya vitabu na akakufuru vyengine, basi amevikufuru vyote. Kwa sababu vitabu hivyo ni maneno ya Allaah. Haijuzu kuamini baadhi yake na kukufuru baadhi ya vyengine. Allaah (Ta´ala) amesema:
أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍۚ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ ۗوَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ
“Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakanusha baadhi yake? Basi hapana malipo kwa anayefanya hayo miongoni mwenu isipokuwa utwevu katika maisha ya dunia na siku ya Qiyaamah watapelekwa kwenye adhabu kali zaidi, na Allaah si Mwenye kughafilika kwa myatendayo.”[3]
Vivyo hivyo kitabu kimoja chenyewe kama chenyewe; ni lazimakuamini yote yaliyomo ndani yake na kuyatendea kazi. Haifai kwetu kufanyia kazi yale yanayoafikiana na matamanio yetu na tukayaacha yale yanayokwenda kinyume na matamanio yetu. Yeyote ambaye atakanusha kitabu kimoja miongoni mwa vitabu vya Allaah, sehemu yake, neno moja au herufi moja ya kitabu, basi amemkufuru Allaah (´Azza wa Jall).
[1]2:285
[2]4:163
[3]2:85
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 129-130
- Imechapishwa: 12/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)