94 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ja´far bin ´Awn ametukhabarisha, kutoka kwa Ibraahiym bin Ismaa´iyl, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Ja´far bin ´Amr bin Umayyah, kutoka kwa baba yake:

” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimtuma peke yake kama jasusi kwenda kwa Quraysh.”

95 – as-Saltw bin Mas´uud ametukhabarisha: Yahyaa bin ´Abdillaah bin Yaziyd bin ´Abdillaah bin Unays ametukhabarisha, kutoka kwa ami yake:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimtuma peke yake katika kikosi.”

96 – Ibn Kaasib ametukhabarisha: Sufyaan bin Hamzah ametukhabarisha: Kathiyr bin Zayd amenihadithia, kutoka kwa at-Twufayl bin Mudrik, kutoka kwa babu yake:

“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimtuma kumleta msichana wake kutoka Makkah.”

97 – al-Huutwiy ametukhabarisha: Ibn Humayd ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin Abiy Daawuud, kutoka kwa Twaawuus, kutoka kwa ´Ammaar bin Yaasir, ambaye amesema:

“Nilikuwa miongoni mwa Maswahabah kumi pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipomuona mtu anayemuelekea. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Je, mnaona chochote?” Wakasema: “Ndiyo, Mtume wa Allaah. Tunamwona mtu anayetuelekea.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Hakuwa na mtu yeyote wa kusuhubiana naye kwa muda wa siku tatu. Chakula pekee alichokuwa nacho ni kile ambacho kimeliwa na farasi wake.” Alipofika tukamsogelea na kusema: “Huyo mtu anatoka wapi?” Akasema: “Sina mtu yeyote wa kusuhubiana naye kwa siku tatu. Chakula pekee nilichokuwa nacho ni kile ambacho kimeliwa na farasi wangu.”

98 – al-Huutwiy ametukhabarisha: Ibn ´Ayyaas ametukhabarisha, kutoka kwa Swadaqah bin ´Abdillaah, kutoka kwa al-Muhaajir bin Habiyb, kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesema:

“Nimewakaripia wale wanazuoni wanaowafuata watenda madhambi. Badala yake ilipasa kwa watenda madhambi wawafuate wanazuoni.”

99 – Wahb bin Baqiyyah ametukhabarisha: Khaalid ametukhabarisha, kutoka kwa Ismaa´iyl, kutoka kwa Qays: Nimemsikia Twalhah bin ´Ubaydillaah akisema:

“Aibu ndogo kwa mtu ni yeye kukaa ndani ya nyumba yake.”

100 – Abu Bakr ametukhabarisha: Husayn bin ´Aliy al-Ju´fiy ametukhabarisha, kutoka kwa Zaa-idah, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin ´Umayr: Bwana mmoja – Abu Bakr alimtaja jina – amenikhabarisha:

“´Abdullaah alimuusia mwanawe ‘Abdur-Rahmaan na akasema: “Nakuusia kumcha Allaah, ikutoshe nyumba yako, udhibiti ulimi wako na ulie juu ya dhambi yako.”

101 – Abu Bakr ametukhabarisha: al-Waliyd bin Muslim ametukhabarisha, kutoka kwa Rawh bin Janaah: Yuunus bin Halbas ametukhabarisha kwamba amewahadithia kuwa amemsikia kuwa Mu´aawiyah amemsimulia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Kheri ni mazowea na shari ni ukaidi.”[1]

[1] Ibn Maajah (221). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3348).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 23-25
  • Imechapishwa: 30/06/2025