at-Twahaawiy (1/512) amesema: Ibraahiym bin Marzuuq ametuhadithia: Abu Rabiy´ah ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa al-Hajjaaj bin Artw-ah, kutoka kwa ´Abdul-Malik, kutoka kwa Sa´iyd bin Fayruuz, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia:
”Wakati wajumbe wa kabila la Thaqiyf walipokuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), walisema: ”Tulimuona akiswali akiwa amevaa viatu viwili vilivyokabiliwa.”
Katika cheni yake wa pokezi kuna al-Hajjaaj bin Artw-ah, ambaye ni mwenye kufanya hadaa. Hata hivyo al-Haythamiy amesema:
”Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw”. Wanaume wake ni wenye kuaminika.”[1]
Mtu anatakiwa kutazama kama inayo njia nyingine au kama al-Hajjaaj ametamka wazi ni nani ameisikia kutoka kwake. Au al-Haythamiy ameichukulia wepesi[2]?
[1] Majma´-uz-Zawaa’id (2/55).
[2] Kwa mujibu wa ´Abdullaah bin Yuusuf l-Hajjaaj bin Artw-ah anakosa jina katika “Zawaa’id-ul-Mu´jamayn”, kama alivyobainisha na matokeo yake al-Haythamiy akaihukumu Hadiyth kama alivyofanya.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 13-14
- Imechapishwa: 02/06/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket