51- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Lau watu wangelijua kuna nini katika adhaana na katika safu ya kwanza na kisha wasipate namna ya kwenda isipokuwa kwa kutambaa, basi angelitambaa.”
52- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wakati kunaponadiwa kwa ajili ya Swalah Shaytwaan hugeuka na kuachia pumzi ili asiweze kusikia adhaana. Wakati adhaana inapokwisha hurudi. Wakati kunapokimiwa kwa ajili ya Swalah hugeuka. Wakati kunapomalizwa kukimiwa hurudi. Hutembea kati ya mtu na nafsi yake na kumwambia: “Fikiria kadhaa! Fikiria kadhaa!” Anamfanya kufikiria vitu ambavyo amesahau mpaka mwishoni asahau ameswali ngapi.”
53- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna jini wala mwanaadamu anayesikia sauti ya muadhini isipokuwa atamshuhudilia siku ya Qiyaamah.”
54- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mnapomsikia muadhini semeni kama anavyosema.”
55- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mnapomsikia muadhini semeni kama anavyosema. Kisha niswalieni. Kwani yule anayeniswalia Swalah mara moja Allaah Anamswalia Swalah kumi kwa hilo. Halafu niombeeni Wasiylah. Hakika ni manzilah Peponi ambayo itapata mmoja katika waja wa Allaah. Ninataraji itakuwa mimi. Atayeniombea Wasiylah atapata Shafaa´ah (uombezi) wangu.”
56- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Muadhini anaposema:
الله أَكْبَرُ اللهُ أَكْبرُ
“Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa” basi mmoja wenu aseme:
الله أَكْبَرُ اللهُ أَكْبرُ
“Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa” na halafu anaposema:
أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا الله
“Nashuhudia kwamba hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah” na aseme:
أَشْهَدُ أَنْ لا إِله إِلا الله
“Nashuhudia kwamba hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah” na halafu anaposema:
أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولاللهُ
”Nashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah” na aseme:
أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً رَسُولاللهُ
”Nashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah” na halafu anaposema:
حَيَّ عَلى الصلاةِ
“Njooni katika Swalah” na aseme:
لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بالله
“Hapana mabadiliko wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah” na halafu anaposema:
حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ
“Njooni katika mafanikio” na aseme:

“Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa” na aseme:

لا إِله إِلا الله
“Hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah” na aseme:
لا إِله إِلا الله
“Hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah” kutoka moyoni mwake, ataingia Peponi.”
57- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anayesema pale anaposikia adhaana:
اللَّهُمَّ ربَّ هَذه الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ والصَّلاَةِ الْقَائِمَةِ آتِ مُحَمَّداً الوسيلة والْفَضِيلَةَ وَابْعَثْهُ مَقَاماً محموداً الذي وَعَدْتَهُ
“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia na Swalah iliosimama! Mpe Mtume Wasiylah na fadhila. Mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo umemuuahidi.”
atapata Shafaa´ah (uombezi) wangu siku ya Qiyaamah.”
58- ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba watu wawili walisema:
“Ee Mtume wa Allaah! Waadhini ni wabora kuliko sisi.” Hivyo akasema: “Semeni kama wanavyosema. Wakati unapomaliza omba na utaitikiwa”.”
59- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Du´aa hairudishwi baina ya adhaana na Iqaamah.”
60- Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mambo mawili hayarudishwi – au ni mara chache yanarudishwa: Du´aa wakati wa adhaana na wakati wa matatizo ambapo watu wanachinjana wao kwa wao.”
- Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 47-51
- Imechapishwa: 21/03/2017

Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 47-51
Imechapishwa: 21/03/2017
https://firqatunnajia.com/12-adhaana-na-mwenye-kuisikia/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)