116. Wanafunzi wanapaswa kubainisha mfumo wa Salaf na kujihadhari na mfumo wa Khawaarij

Swali 116: Kipi unachowanasihi wanafunzi?

Jibu: Nawanasihi wawatakie watu mema kwa ajili ya Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), viongozi wa waislamu na watu wa kawaida, kama alivyowaamrisha jambo hilo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah pia amechukua ahadi kutoka kwao pale aliposema:

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ

“Wakati alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu [akawaambia:] “Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha. Lakini walikitupa nyuma ya migongo yao na wakakibadilisha kwa thamani ndogo. Basi ubaya ulioje kwa yale wanayoyanunua!”[1]

Wanafunzi wanasihi na kubainisha kwa mujibu wa mfumo wa Qur-aan, Sunnah kwa ufahamu wa Salaf.

Vilevile wajihadhari na mfumo Khawaarij na Mu´tazilah ambao wanahimiza uasi dhidi ya viongozi wa waislamu, kuwakashifu, kutumia ususuwavu na kuwashtua watu[2]. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Fanyeni wepesi na msifanye ugumu. Toeni bishara njema na wala msikimbize. Hapana vyenginevyo mmtumwa hali ya kuwa ni wenye kuwepesisha, na hamkutumwa hali ya kuwa ni wenye kutia ugumu.”[3]

Haya ndio ambayo nawanasihi wanafunzi na khaswakhaswa walinganizi.

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake, Maswahabah zake na wale watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.

[1] 3:187

[2] Sambamba na hilo wakidai kuwa wanaamrisha mema na kukataza maovu. Kutokana na hoja hiyohiyo ndio ilikuwa sababu ya kuuliwa khaliyfah mwongofu ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh). Kwa sababu fahamu yao ni pungufu na utambuzi wao ni mchache. Ahl-us-Sunna wal-Jamaa´ah wamethibitisha kwamba mambo haya sio katika kuamrisha mema na kukemea maovu, bali ni mfumo wa Khawaarij ambao Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametutahadharisha nao.

[3] al-Bukhaariy (69) na Muslim (1733).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 270-271
  • Imechapishwa: 26/08/2024
  • Taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy