Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Kisha akasema:

“Hakika mimi nimekuacheni kile ambacho endapo mtashikamana nacho basi hamtopotea baada yangu; Kitabu cha Allaah.”[1]

MAELEZO

Hii ni miongoni mwa neema ya Allaah. Hakutuacha tukachanganyikiwa wakati wa tofauti. Ametupa njia sahihi tutayopita juu yake. Lakini hili linahitaji mambo matatu:

1 – Elimu sahihi na si janjajanja. Huwezi kushika njia hii usiposoma na ukajifunza haki kutokamana na batili.

2 – Subira na uimara. Usiyumbeyumbe, pasi na kujali kile kitachokupata. Unatakiwa kusubiri juu ya chochote kitachokupata.

3 – Usidanganyike na wingi. Badala yake unatakiwa kushikamana na haki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

” Hakika mimi nimekuachieni yale ambayo endapo mtashikamana nayo basi hamtopotea; Kitabu cha Allaah na Sunnah zangu.”[2]

Bi maana Qur-aan na Sunnah ambazo ni zile Hadiyth Swahiyh. Hakusema kuwa ametuachia akili zetu, fikira zetu, theolojia, mijadala na falsafa – amesema:

”Kitabu cha Allaah na Sunnah zangu.”

Hii ndio njia ya uokozi. Hili linamlazimu muislamu kushikamana na Qur-aan na Sunnah.

[1] Muslim (1218) na Abu Daawuud (1905).

[2] Maalik (1594) na al-Haakim (1/171).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 167-168
  • Imechapishwa: 10/09/2024