5 – Wanasema eti kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni miongoni mwa Bid´ah nzuri, kwa sababu maana yake ni kuonesha shukurani kwa kule kuumbwa kwa mtukufu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunajibu hilo kwa kusema kwamba hakuna kitu chochote kizuri katika Bid´ah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote atakayezua kitendo kisichokuwa katika amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika ya kila Bid´ah ni upotevu.”[2]
Amehukumu kwamba Bid´ah zote ni upotevu. Huyu mtetezi anasema kuwa sio kila Bid´ah ni potevu na kwamba zipo Bid´ah ambazo ni nzuri. Haafidhw Ibn Rajab amesema katika maelezo yake ya “al-Arba´iyn an-Nawawiyyah”:
“Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kila Bid´ah ni upotevu.”
ni miongoni mwa maneno mafupi yenye maana pana. Hakuna chochote kinachobaguliwa humo. Ni msingi mkubwa miongoni mwa misingi ya dini. Ni sawa na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote atakayezua kitendo kisichokuwa katika amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”
Kwa hiyo kila atakayezua kitu akakinasibisha na dini bila kuwa na msingi ndani ya dini, basi ni upotofu na dini haina uhusiano nacho. Ni mamoja iwe ni katika mambo ya imani, matendo au maneno ya ndani au ya nje.”[3]
[1] al-Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).
[2] Ahmad (16692) at-Tirmidhiy (2676).
[3] Jaamiy´-ul-´Uluum wal-Hikam, uk. 233
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 152-154
- Imechapishwa: 06/09/2025
5 – Wanasema eti kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni miongoni mwa Bid´ah nzuri, kwa sababu maana yake ni kuonesha shukurani kwa kule kuumbwa kwa mtukufu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunajibu hilo kwa kusema kwamba hakuna kitu chochote kizuri katika Bid´ah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote atakayezua kitendo kisichokuwa katika amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika ya kila Bid´ah ni upotevu.”[2]
Amehukumu kwamba Bid´ah zote ni upotevu. Huyu mtetezi anasema kuwa sio kila Bid´ah ni potevu na kwamba zipo Bid´ah ambazo ni nzuri. Haafidhw Ibn Rajab amesema katika maelezo yake ya “al-Arba´iyn an-Nawawiyyah”:
“Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kila Bid´ah ni upotevu.”
ni miongoni mwa maneno mafupi yenye maana pana. Hakuna chochote kinachobaguliwa humo. Ni msingi mkubwa miongoni mwa misingi ya dini. Ni sawa na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote atakayezua kitendo kisichokuwa katika amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”
Kwa hiyo kila atakayezua kitu akakinasibisha na dini bila kuwa na msingi ndani ya dini, basi ni upotofu na dini haina uhusiano nacho. Ni mamoja iwe ni katika mambo ya imani, matendo au maneno ya ndani au ya nje.”[3]
[1] al-Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).
[2] Ahmad (16692) at-Tirmidhiy (2676).
[3] Jaamiy´-ul-´Uluum wal-Hikam, uk. 233
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Huquwq-un-Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bayn al-Ijlaal wal-Ikhlaal, uk. 152-154
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/11-maulidi-ni-katika-bidah-nzuri/