Miongoni mwa haki za wanandoa wakati wa mkataba wa ndoa ni pamoja na mwanamke apate mahari sahali. Yasiwe ni yenye kupita mipaka. Mume asitoe zaidi ya kile anachoweza. Moja katika mambo yanayochangia wanandoa kuwa na furaha ni mume kutokalifishwa na madeni na shida zake. Asihisi ya kwamba mwanamke anayeishi naye na kuchangia naye shuka moja ndio sababu ya shida zake asizoweza kuzitunza. ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye alipata msukumo na ni mmoja katika makhaliyfah waongofu amesema:
“Msipetuke mipaka kwa mahari ya wanawake. Lau yangelikuwa yanaleta utukufu katika dunia na ucha-Mungu kwa Allaah, basi Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angelifanya hivo kabla yenu. Hakumpa zaidi ya Uqiyah kumi na mbili (dirhamu mia tano) mmoja katika wake zake na wala hakumpa zaidi ya hivo mmoja katika wasichana zake. Pengine mwanaume akakereka na mahari ya mwanamke wake mpaka akaanza kumchukia na kusema: “Nilisumbuka kwa ajili yako.“[1]
[1] Ibn Maajah (1887), an-Nasaaiy (3349), Ahmad (1/40-41), Abu Daawuud (1799) na at-Tirmidhiy mpaka ”Uqiyah kumi na mbili”. at-Tirmidhiy amesema: ”Ni nzuri na Swahiyh.”
- Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 18-19
- Imechapishwa: 24/03/2017
Miongoni mwa haki za wanandoa wakati wa mkataba wa ndoa ni pamoja na mwanamke apate mahari sahali. Yasiwe ni yenye kupita mipaka. Mume asitoe zaidi ya kile anachoweza. Moja katika mambo yanayochangia wanandoa kuwa na furaha ni mume kutokalifishwa na madeni na shida zake. Asihisi ya kwamba mwanamke anayeishi naye na kuchangia naye shuka moja ndio sababu ya shida zake asizoweza kuzitunza. ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye alipata msukumo na ni mmoja katika makhaliyfah waongofu amesema:
“Msipetuke mipaka kwa mahari ya wanawake. Lau yangelikuwa yanaleta utukufu katika dunia na ucha-Mungu kwa Allaah, basi Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angelifanya hivo kabla yenu. Hakumpa zaidi ya Uqiyah kumi na mbili (dirhamu mia tano) mmoja katika wake zake na wala hakumpa zaidi ya hivo mmoja katika wasichana zake. Pengine mwanaume akakereka na mahari ya mwanamke wake mpaka akaanza kumchukia na kusema: “Nilisumbuka kwa ajili yako.”[1]
[1] Ibn Maajah (1887), an-Nasaaiy (3349), Ahmad (1/40-41), Abu Daawuud (1799) na at-Tirmidhiy mpaka ”Uqiyah kumi na mbili”. at-Tirmidhiy amesema: ”Ni nzuri na Swahiyh.”
Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 18-19
Imechapishwa: 24/03/2017
https://firqatunnajia.com/11-mahari-yanatakiwa-kuwa-mepesi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)