11. Kufanya bidii ya ziada katika Ramadhaan

Enyi waja wa Allaah! Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya juhudi katika mwezi huu zaidi kuliko miezi mingine, ingawa alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwenye juhudi katika ´ibaadah wakati wote. Lakini katika mwezi huu alikuwa akiacha baadhi ya mashughuliko ambayo kiasili nayo ni ´ibaadah, lakini akiyaacha yaliyo mema kwa ajili ya yaliyo bora zaidi. Salaf walikuwa wakimfuata katika hilo ambapo wakaubagua mwezi huu kwa uangalizi mkubwa zaidi, wakajitenga kwa matendo mema, wakauhuisha usiku wake kwa kisimamo cha usiku, mchana wake kwa funga, dhikr na kusoma Qur-aan na wakaihuisha misikiti kwa hayo. Kwa hiyo tulinganishe hali yetu na hali yao na tujiulize kiwango cha hisia zetu kwa mwezi huu. Tuelewe kuwa, kama vile thawabu zinavyoongezwa ndani yake, ndivyo pia madhambi yanavyozidishiwa uzito na adhabu yake kuwa kubwa. Basi na tumche Allaah (Subhaanah) na tuyatukuze matukufu Yake:

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ

“Ndio hivyo iwe na yeyote anayetukuza vitukufu vya Allaah, basi hivyo ni kheri kwake mbele ya Mola wake.”[1]

[1] 22:30

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 18
  • Imechapishwa: 02/02/2026