Haafidhw ´Abdul-Ghaniy al-Maqdisiy al-Hanbaliy (Rahimahu Allaah) amesema:
186 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kuleni daku. Kwani hakika katika daku kuna baraka.”[1]
MAELEZO
Katika Hadiyth Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha na kuhimiza kula daku. Daku ni chakula cha mfungaji katika mwisho wa usiku, wakati wa alfajiri kabla ya kuchomoza kwa jua. Kimepewa jina hili kwa sababu ya kupatikana kwake katika wakati huu. Allaah (Ta´ala) amesema:
”wal mustaghfirina…haar”
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekiita:
”Chakula cha jioni kilichobarikiwa.”[2]
Ameifanya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa tofauti kati ya watu wa Kitabu na waislamu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kipambanuzi kati ya swawm yetu na swawm ya watu wa Kitabu ni kula daku.”[3]
Baadhi ya Maswahabah wamekiita kuwa ni mafanikio. Imepokelewa kwamba Abu Dharr (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“… ilipofika usiku wa tatu, aliwakusanya familia yake na wake zake, akatuswalisha mpaka tulipoanza kuogopa kukosa mafanikio.” Nikasema: ”Ni nini mafanikio?” Akasema: “Ni daku.”[4]
Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kuleni daku.”
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kula daku. Amri inapelekea katika uwajibu. Maafikiano yanasema kuwa daku inapendeza, kama alivosema Ibn-ul-Mundhir:
”Wameafikiana juu ya kwamba daku imependekezwa.”
Imeondolewa kutoka kuwa wajibu kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliunganisha swawm pamoja na Maswahabah zake na hakula daku.
Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kwani hakika katika daku kuna baraka.”[5]
Kuna dalili ya fadhilah na baraka ya kula daku na kwamba ni jambo linalopendekezwa.
[1] al-Bukhaariy (1923) na Muslim (1095).
[2] Ahmad (17152), Abu Daawuud (2344), an-Nasaa´iy (2163), Ibn Khuzaymah (1938) na Ibn Hibbaan (3465). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (7043).
[3] Muslim (1096).
[4] Ahmad (21419), Abu Daawuud (1375), at-Tirmidhiy (806), an-Nasaa´iy (1605) na Ibn Maajah (1327). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Khuzaymah (2206), Ibn Hibbaan (2547) na al-Albaaniy katika “Mishkaat-ul-Maswaabih” (1298).
[5] al-Bukhaariy (1923) na Muslim (1095).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/439-440)
- Imechapishwa: 23/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket