117 – Nu´aym bin Hammaad amesimulia kuwa amemsikia Nuuh al-Jaamiy akisema:

”Nilikuwa kwa Abu Haniyfah pale mwanzoni alipodhihiri. Akaja mwanamke mmoja kutoka Tirmidh, ambaye alikuwa akiketi na al-Jahm, akafika Kuufah na akaenda kwake. Nafikiri kulikuwa watu wasiopungua elfu kumi ambao walikuwa wakilingania katika ´Aqiydah ya mwanamke huyo. Kukasemwa: ”Hapa kuna bwana mmoja akiitwa Abu Haniyfah anayesoma akili. Mwendee.” Akamwendea na kusema: ”Wewe ndiye ambaye unawafunza watu mambo na umeacha dini yako? Yuko wapi Mola wako unayemwabudu?” Akamnyamazia. Zikapita siku saba hakumjibu. Kisha akatutokea. Alikuwa ameandika karatasi na kusema: ”Allaah (´Azza wa Jall) yuko juu ya ´Arshi na sio ardhini.” Bwana mmoja akamwambia: ”Unasemaje juu ya maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ٌ

”Naye Yu pamoja nanyi popote mlipo.”[1]

Akasema: ”Ni kama unavyomwandikia mtu kwamba uko pamoja naye ilihali wewe uko mbali naye.”

Ameipokea al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa´ was-Swifaat”[2], ambaye amesema:

”Abu Haniyfah amepatia katika yale aliyosema kwamba Allaah hayuko ardhini, kuifasiri Aayah kwa namna hiyo na kufuata dalili kuhusiana na kwamba Allaah yuko juu ya mbingu.”

[1] 57:4

[2] Udhahiri ni kwamba mtunzi (Allaah amsamehe yeye na sisi) kwamba al-Bayhaqiy amenyamazia cheni ya wapokezi ya kisa hiki. Mambo sivyo. Ameashiria juu ya udhaifu wake pale aliposema:

”Ikiwa hayo yamesihi kutoka kwake.”

Ni vipi yatasihi? Kimesimuliwa na Nuuh al-Jaamiy ambaye ametuhumiwa uundaji. Baadhi wamefikia mpaka kusema kwamba amekusanya kila kitu isipokuwa tu ukweli. Nu´aym ni dhaifu na baadhi wamemtuhumu. Ingelikuwa ni vyema kwa mtunzi kubainisha jambo hilo na asitoe nafasi kwa adui kumsema vibaya, kama alivofanya al-Kawthariy katika “Takmilat-ur-Radd ´alaa Nuuniyyah Ibn-il-Qayyim”, uk. 179.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 135
  • Imechapishwa: 14/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy