Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Pindi watu hawa wanapolinganiwa katika Qur-aan na Sunnah wanavipa mgongo na huku wanadai kuwa makusudio yao ni mazuri na wanachotaka ni kuoanisha kati ya dalili za kiakili na dalili za kinakili. Kisha isitoshe nyingi katika hoja zao tata ambazo wao huziita kuwa ni dalili si jengine isipokuwa ni kuwafuata kichwa mchunga masanamu katika washirikina na wasabai; baadhi ya warithi wao ambao wameamrishwa kuwakufuru au baadhi ya watu wenye nadharia moja kama wao:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha.”[1]

كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ

“Watu walikuwa ummah mmoja kisha Allaah akawatuma Mitume hali ya kuwa ni wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu kati ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo.”[2]

MAELEZO

Wanatheolojia na wanafalasafa hawa, ambao wanachukua I´tiqaad zao kutoka katika isiyokuwa Qur-aan na Sunnah, wanafanana na wanafiki waliokuwa wakiishi wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Qur-aan imeteremshwa na inafanya kazi mpaka katika zama za mwisho na si katika zama za mwanzo peke yake. Mfumo huu ambao wamechukua, kwa njia ya kurejea katika akili na kuipuuza Qur-aan na Sunnah, wameichukua kutoka kwa masanamu yao na maadui wa Mitume, wakiwemo wagiriki au wafursi. Au wamewafata kichwa mchunga watu wasiokuwa na utambuzi na wasiofikiria ambao wamewafuata kibubusa waliotangulia. Wanasoma na mantiki kana kwamba ni jambo ambalo halitakiwi kupingwa kabisa. Hawarejei katika Qur-aan na Sunanh. Katika ´Aqiydah wanasoma mantiki na wanadai kuwa hiyo ni dalili ya yakini tofauti na Qur-aan na Sunnah, ambavyo ni udhahiri tu usiyofahamisha juu ya yakini. I´tiqaad zao katika shule, vyuo vikuu vyao na vitivo vyao vimjengeka juu ya mantiki. Shari ipo na bali inaongezeka.

Imani sio madai tu. Imani ni kutamka kwa ulimi, kuamini moyoni na matendo ya viungo. Ni vipi mtu atasema kuwa ni muumini kisha ahukumiane na kitu kingine isiyokuwa Qur-aan na Sunnah? Angelikuwa kweli ni muumini, basi angelihukumiana na Qur-aan na Sunnah. Matendo yake yanapingana na maneno yake na yanajulisha yale anayoamini moyoni kwamba si sahihi kuhukumiana na Qur-aan na Sunnah. Aayah hizi ni dalili inayoonyesha kuwa uongofu pekee unapatikana katika Vitabu vilivyoteremshwa, ni mamoja ni Tawraat, Injiyl, Zabuur au Qur-aan. Lakini Kitabu cha mwisho ni Qur-aan ndio inayofanya kazi mpaka kisimame Qiyaamah. Kwa ajili hiyo inatakiwa kuhukumu kwa Qur-aan pekee katika mambo ya ´Aqiydah na makinzano mengine. Sunnah ni yenye kuifuata Qur-aan. Kuhusu ambaye anahukumu kwa isiyokuwa Qur-aan hawezi hata siku moja kufikia katika ufumbuzi, isipokuwa tu dhuluma, mkanganyiko na vurugu, ni mamoja inahusiana na maneno, mambo ya I´tiqaad au magomvi. Hakuna ufumbuzi mwingine isipokuwa kuhukumu kwa Qur-aan na Sunnah.

[1] 4:65

[2] 2:213

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 153-156
  • Imechapishwa: 04/09/2024