Swali 105: Ni kina nani Jamaa´at-ut-Tabliygh? Wanafuata mfumo gani? Je, inafaa kujiunga nao na kutoka nao kwa ajili ya kulingania ikiwa ni wanafunzi na wako na ´Aqiydah sahihi, kama watu wa nchi hii?
Jibu: Kundi pekee ambalo ni lazima kujiunga nalo, kwenda nalo na kufanya kazi nalo ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao wanapita juu ya yale aliyokuwa akipita juu yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Kuhusu mengine yote yanayopingana nayo ni wajibu tujitenge nayo.
Ni kweli kwamba tunapaswa kuwalingania kwa Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini sio kujiunga nao, kutoka nao na kutembea juu ya mipango yao ilihali tunajua kwamba hawako katika njia sahihi. Haijuzu kufanya hivo, kwa sababu itakuwa ni kusimama upande wa kundi ambalo sio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 247-248
- Imechapishwa: 13/08/2024
- Taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)