6- Alimwamrisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aseme:

اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنَ الْخَيْرِ كُلِّهِ عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الشَّرِّ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآَجِلِهِ مَا عَلِمْتُ مِنْهُ، وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ ،اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَأَلَكَ عَبْدُكَ وَ رَسولُكَ مُحَمَّدٌ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَاذَ مِنْهُ عَبْدُكَ وَرَسولُكَ مُحَمَّدٌ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، و أسألُكَ ما قَضَيْتَ لي مِنْ أمرٍ أن تَجْعَلَ عاقِبَتَهُ لي رشداً

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba mema yote, [hapa duniani na huko Aakhirah], ninayoyajua na nisiyoyajua. Na najilinda Kwako na shari zote, [hapa duniani na huko Aakhirah], ninazozijua na nisizozijua. Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba Pepo na kila kauli au kitendo kinachokaribisha nayo. Najilinda Kwako na Moto na kila kauli na kitendo kinachokaribisha nao. Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kheri zote alizokuomba mja na Mtume Wako Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na najilinda Kwako na shari zote alizojilinda nazo mja na Mtume Wako Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na nakuomba yale yote uliyonihukumia Uyafanye matokeo yake yawe ya uongofu.”[1]

[1] Ahmad, at-Twayaalisiy, al-Bukhaariy katika ”al-Adab al-Mufrad”, Ibn Maajah na al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Nimeiweka katika ”as-Swahiyhah” (1542).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 161
  • Imechapishwa: 10/01/2019