101. Akili zetu ni zenye upungufu na zinatofautiana

Wanachomaanisha ni kwamba yale yanayokanushwa na akili, basi yanatakiwa kukanushwa. Kwa mujibu wao akili ndio dalili. Maana yake ni kwamba tunabaki katika hali ya kuchanganyikiwa, kwamba Allaah ametuacha na wala hakutubainishia jambo hili. Kwa msemo mwingine ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewaacha waja Wake na wala hakuwabainishia njia ya haki na ya sawa. Ikiwa Allaah ametuacha tuzitegemee akili zetu wenyewe; swali ni je: akili zote zinalingana? Akili ni zenye kutofautiana na makinzano. Ndio maana utaona namna ambavyo watu wako katika mikanganyo na makinzano. Mmoja anakanusha, mwingine anathibitisha. Mwingine anatia upotofuni, mwingine anakufurisha na mwingine anatia katika ufuska. Hili ni kwa sababu akili za watu ni zenye kutofautiana. Haziko katika kiwango kimoja. Jengine ni kwamba ni zenye upungufu. Hazifahamu mambo yaliyofichikana yaliyopita na yanayokuja huko mbele. Akili za watu ni zenye upungufu, zenye vurugu na zenye makinzano.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 146
  • Imechapishwa: 02/09/2024