Tambua kwamba asili ya kila hukumu ya kishari´ah ni Qur-aan Tukufu. Qur-aan ndio chimbuko la misingi yote, chemchem ya marejeo yote na msingi mkuu unaojumuisha misingi mingine yote. Haiwezekani kuwepo hukumu yoyote ya Kishari´ah isipokuwa irejee kwake na itokane nayo. Hata Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asili yake ni Kitabu cha Allaah (Ta´ala), kwa kuwa Sunnah ni ufafanuzi wa yaliyokuja kwa ujumla ndani yake, ni kubainisha yaliyoachwa bila ufafanuzi na ni njia miongoni mwa njia za kutoa hukumu kutoka ndani yake. Kila Sunnah, mtafiti mwenye ujuzi akichunguza asili yake, basi atakuta iko ndani ya Kitabu cha Allaah (Ta´ala), ikijulishwa ima kwa maandishi ya moja kwa moja ya Aayah, kwa dhahiri yake, kwa maana inayoeleweka, kwa dalili ya ishara yake, kwa ujumla wake na njia nyinginezo za kutoa hukumu ambazo wanazuoni huzijua na baadhi yake hutajwa katika fani ya misingi ya Fiqh. Ukipata kulifahamu hilo, basi suala letu hili la kupangusa juu ya soksi msingi wake uko katika Qur-aan Tukufu, ima kutokana na ujumla wa kupaka uliyotajwa katika Aayah ya wudhuu´ au kutokana na ujumla mwingine katika Aayah nyingine. Kuhusu ujumla wa kwanza, ushahidi wake ni kusoma kwa namna hii:
وَأَرْجُلِكُمْ
”… na miguu yenu… ”[1]
Kwa dhahiri yake ni wajibu kupangusa juu ya miguu kwa mujibu wa kisomo hicho, kama jinsi hayo yamepokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas, Anas, ´Ikrimah, ash-Sha´biy, Qataadah, Ja´far as-Swaadiq na wanazuoni wa kizazi chake – Allaah awe radhi nao wote kwa pamoja! Kwa mujibu wa madhehebu ya maimamu hawa maana ya Aayah ni kuwajibika kupangusa juu ya miguu, ima moja kwa moja au juu ya kilichoko juu yake kama vile soksi za ngozi, soksi za kawaida au vitambaa vya kufunika miguu[2]. Hivyo kwa mujibu wa kisomo hiki inaonekana wazi kwamba Aayah ni chimbuko la Sunnah katika suala hili.
Ama kwa mujibu wa kauli ya wanazuoni wengi Aayah inasomwa namna hii:
وَأَرْجُلَكُمْ
”… na miguu yenu… ”
Kwa maana nyingine ni lazima kuosha miguu. Katika hali hiyo chimbuko la kupaka juu ya soksi lipo ndani ya Qur-aan, kwa maana katika Aayah za jumla, ikiwa ni pamoja na:
وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمْ عَنْهُ فَٱنتَهُوا۟ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ
”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni. Mcheni Allaah, hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.”[3]
لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَا
“Hakika mna kigezo chema kwa Mtume wa Allaah kwa yule mwenye kumtaraji Allaah na siku ya Mwisho.”[4]
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah na atakusameheni dhambi zenu na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[5]
وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ
”Mtiini Allaah na mtiini Mtume!”[6]
Na mifano mingine isiyohesabika. Njia za kutoa hukumu zimekuwa nyingi. Baadhi yake hupata uzito zaidi kwa nguvu ya mtawanyiko wake na uhusiano wake. Njia za kutoa uzito hazifichiki kwa wale wanazuoni waliobobea katika elimu.
[1] 5:6
[2] Shîy´ah wameenda kinyume katika hili. Hawaonelei kufaa kupangusa juu ya soksi za ngozi, soksi za kawaida wala vitambaa vya kufunika miguu.
[3] 59:7
[4] 33:21
[5] 3:31
[6] 64:12
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 21-22
- Imechapishwa: 02/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 21-22
Imechapishwa: 02/04/2026
https://firqatunnajia.com/10-kupangusa-juu-ya-soksi-ndani-ya-qur-aan/