49 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiomba du´aa kwa kusema:
أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْبُخْلِ، وَالْكَسَلِ، وَأَرْذَلِ الْعُمُرِ، وَعَذَابِ الْقَبْرِ، وَفِتْنَةِ الدَّجَّالِ، وَفِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ
“Najilinda kwa Allaah kutokana na ubakhili, uvivu na umri wenye udhalili, adhabu ya kaburi, mtihani wa ad-Dajjaal, mtihani wa uhai na wa kifo.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْعَجْزِ وَالْكَسَلِ، وَالْجُبْنِ وَالْهَرَمِ والْبُخْلِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ، وَمِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا َالْمَمَاتِ
“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokana na kushindwa, uvivu, woga, ukongwe, ubakhili na najilinda Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, kutokana na mtihani wa uhai na wa kifo.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْهَمِّ وَالْحَزَنِ، وَالْعَجْزِ وَالْكَسَلِ، وَالْجُبْنِ وَالْبُخْلِ، وَضَلَعِ الدَّيْنِ وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ
“Ee Allaah! Hakiki mimi najilinda Kwako kutokana na hamu, huzuni, kushindwa, uvivu, woga, ubakhili, uzito wa deni na kushindwa na wanaume.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْكَسَلِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ الْجُبْنِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ الْهَرَمِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ الْبُخْلِ
“Ee Allaah! Hakiki mimi najilinda Kwako kutokana na uvivu, najilinda Kwako kutokana na woga, najilinda Kwako kutokana na ukongwe na najilinda Kwako kutokana na ubakhili.”[1]
Kuna maafikiano juu yake.
MAELEZO
Hadiyth hizi zinafahamisha usuniwaji wa kujilinda kwa Allaah kutokana na mambo haya. Ni du´aa tukufu ambazo zimekusanya maneno. Zimesuniwa kusomwa ndani ya swalah na nje yake.
Ubakhili ni kule kuzuia yale yanayokuwajibikia.
Uvivu ni kule kuhisi uvivu wa mambo ya kheri licha ya kwamba mtu ana uwezo wa kuyafanya.
Kushindwa ni kuacha kitu kwa sababu ya kutokiweza.
Umri wenye udhalili ni ule ambao ni mbaya zaidi. Nako ni kule kuchanganyikiwa akili mwishoni mwa umri.
Mtihani wa uhai ni ile mitihani inayokuwa katika maisha katika mambo yenye utata na matamanio.
Mtihani wa kifo ni ule unaokuwa wakati wa kutaka kufa ambapo mtu anatiwa katika mtihani kwa kujiliwa na shaytwaan na kumtahini. Shaytwaan humzungumzisha maneno ya batili au kumzuia kutamka shahaadah.
Woga ni ule unaomzuia mtu kufanya mambo ya kheri, ingawa ana uwezo juu yake, kwa kuogopa asije kufikwa na jambo.
[1] al-Bukhaariy (4707), (6369) na (6371) na Muslim (2706).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 55-56
- Imechapishwa: 14/10/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 55-56
Imechapishwa: 14/10/2025
https://firqatunnajia.com/10-duaa-ya-kujilinda-kwa-allaah-na-ubakhili-uvivu-umri-dhalili-n-k/