10. Du´aa baada ya kumaliza kutawadha

  Download

13-

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ

“Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa pekee hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na ni Mtume wake.”[1]

14-

اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِنَ التَّوَّابِينَ وَاجْعَلْنِي مِنَ الْمُتَطَهِّرِينَ

“Ee Allaah! Nijaalie kuwa katika wenye kutubia na nijaalie kuwa katika wenye kujitwaharisha.”[2]

15-

سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَيْكَ

“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah, na himdi zote ni Zako. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe. Nakuomba msamaha na natubia Kwako.”[3]

[1] Muslim (234).

[2] at-Tirmidhiy (55). Tazama “Swahiyh at-Tirmidhiy” (01/18).

[3] an-Nasaa´iy katika “´Amal-ul-Yawm wal-Laylah”, uk. 173. Tazama “Irwaa´-ul-Ghaliyl” (01/135) na (03/94).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 23/06/2018