Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Kumuamini Allaah ina maana ni pamoja na kuamini yale aliyojieleza Mwenyewe ndani ya Kitabu Chake na kwa yale aliyomueleza kwayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bila ya upotoshaji, ukanushaji, kuzifanyia namna wala kufananisha. Bali wao wanaamini yafuatayo kuhusiana na Allaah (Subhaanah):
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)
Hawakanushi kutoka Kwake yale ambayo amejisifu Mwenyewe na wala hawapotoshi maana ya maneno kuyatoa mahala pake. Hawaharibu majina ya Allaah na Aayah Zake. Hawaainishi maana Yake halisi, hawazifananishi na kuzilinganisha sifa Zake na sifa za viumbe Wake. Hakika Yeye (Subhaanah) hana mshirika wala mwenza na wala halinganishwi na viumbe Wake (Subhaanahu wa Ta´ala).
Kwani hakika Yeye (Subhaanah) ni mjuzi zaidi wa kujijua Mwenyewe na wengine na ni mkweli zaidi wa mazungumzo na maneno yaliyo bora na ya wazi kuliko Viumbe Vyake.
MAELEZO
Kumuamini Allaah ina maana ni pamoja na kuamini yale aliyojieleza Mwenyewe… – Allaah mtu kuamini yale majina ambayo Allaah amejiita kwayo, kwa mfano al-Hakiym [Mwingi wa hekima], al-´Aziyz [Mshindi], Rawuf [Mpole], ar-Rahiym [Mwenye kurehemu], al-Qadiyr [Muweza] na mengineyo. Vilevile mtu kuamini yale majina na sifa ambazo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemsifu kwazo katika Hadiyth Swahiyh. Ni wajibu kumthibitishia nayo Allaah. Kwa mfano yaliyokuja katika Hadiyth Swahiyh:
“Allaah anawacheka watu wawili ambapo mmoja wao kamuua mwenzake. Halafu wote wawili wanaingia Peponi.”[1]
“Hakika Mola Wangu leo amekasirika hasira ambayo hajapatapo kukasirika namna yake hapo kabla na hatokasirika mfano wake baada yake.”[2]
Bi maana siku ya Qiyaamah.
Kuna sifa nyenginezo nyingi za Allaah (Jalla wa ´Alaa) ambazo zimetajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah takasifu. Ahl-us-Sunnah wanaziamini na wakati huohuo wanaziitakidi. Wanaamini kuwa hakuna anayelingana Naye, hana mwenza wala hana mshirika. Vilevile halinganishwi na viumbe Vyake (Subhaanahu wa Ta´ala). Yeye ana majina mazuri na sifa kuu. Ahl-us-Sunnah hawafananishi sifa Zake na sifa za viumbe Vyake (Jalla wa ´Alaa). Bali wanajua kuwa sifa Zake zinalingana na Yeye na hazifanani na sifa za viumbe Vyake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hana mwenye kulingana Naye:
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua mwenye jina kama Lake?” (19:65)
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“Na wala hana yeyote anayefanana [kulingana] Naye.” (112:04)
فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
“Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua [kuwa hana].” (02:22)
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanathibitisha sifa na majina ya Allaah kwa njia inayolingana Naye (Subhaanahu wa Ta´ala). Hawazipingi sifa Zake na hawayapotosho maneno kuyaondosha mahala pake stahiki. Bali wao wanaamini majina na sifa zote zilizotajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah kwa njia inayolingana na Allaah.
[1] al-Bukhaariy (2826) na Muslim (1890).
[2] al-Bukhaariy (3340) na Muslim (194).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 16-17
- Imechapishwa: 16/10/2024

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 16-17
Imechapishwa: 16/10/2024
https://firqatunnajia.com/10-ahl-us-sunnah-wanaamini-majina-na-sifa-za-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)