1- Hadiyth imeonyesha kwamba Abu Qataadah alilipa deni hili baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumswalia maiti. Hapa kuna mushkili. Imesihi kutoka kwa Abu Qataadah huyohuyo kwamba alililipa kabla ya kumswalia, kama itavyokuja katika masuala ya 51 ukurasa wa (02/75). Kama kisa hicho hakitafasiriwa kwamba vilitokea viwili basi itambulike kwamba upokezi wa Abu Qataadah ni sahihi zaidi kuliko Hadiyth ya Jaabir. Kwa sababu ndani yake yumo ´Abdullaah bin Muhammad ´Aqiyl ametiwa dosari. Ni mwenye Hadiyth nzuri kwa yale ambayo hakuna wa kwenda kinyume naye. Akipatikana anayekwenda kinyume naye basi yeye si hoja. Allaah ndiye mjuzi zaidi.
2- Hadiyth hizi zimeonyesha kuwa maiti ananufaika kwa kule kumlipia deni lake ijapokuwa hayakulipwa na mtoto wake na kwamba kumlipia kunamwondoshea adhabu. Ni miongoni mwa jumla ya mambo maalum kwa sababu ya ueneaji wa maneno Yake (Tabaarak wa Ta´ala):
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
“Mtu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi.”[1]
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu… “
Hadiyth hii imepokelewa na Muslim na al-Bukhaariy katika “al-Adab al-Mufrad” na Ahmad.
Lakini kumlipia deni lake ni kitu kimoja na kumtolea swadaqah ni kitu kingine. Jambo la kumlipia deni ni maalum kuliko swadaqah. Baadhi yao wamenukuu maafikiano juu ya kwamba swadaqah ni yenye kumfikia maiti moja kwa moja. Jambo hilo likisihi[2], vinginevyo Hadiyth zilizopokelewa juu ya kumtolea swadaqah maiti zimepokelewa zikionyesha mtoto kuwatolea swadaqah wazazi wake. Mtoto huyo anaingia katika chumo la wazazi wawili kwa dalili ya Hadiyth. Kwa hivyo haijuzu kumlinganisha mtu kando na wazazi wawili. Kwa sababu ni kipimo kinachokwenda kinyume, kama inavyodhihiri. Wala hakuna kipimo cha kulinganisha kutoa swadaqah juu ya kulipa deni. Kwa sababu ni lenye kuenea zaidi, kama tulivyotaja.
Ubainifu zaidi wa masuala haya utakuja katika masuala ya 117.
[1] 53:39
[2] Halikusihi, kama itavyokuja ukaguzi wake.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 28
- Imechapishwa: 30/12/2019

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 28
Imechapishwa: 30/12/2019
https://firqatunnajia.com/1-hadiyth-imeonyesha-kwamba-abu-qataadah-alilipa-deni-hili-baada-ya-mtume-swalla-allaahu-alayhi-wa-sallam-kumswalia-maiti-hapa-kuna-mushkili-imesihi-kutoka-kwa-abu-qataadah-huyohuyo-kwamba/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)