Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah ambaye hakuwajaalia wachaji taabu katika dini na amewataka wepesi wala hakuwataka uzito – Naye ni Mwenye kurehemu kuliko warehemuo wote. Swalah na salamu zimshukie Nabii wa rehema, aliyetumwa kwa dini ya uongofu iliyo nyepesi, rahisi na yenye kusamehe, iliyofutiwa mizigo na pingu zilizokuwa juu ya waliotangulia – bwana wetu Muhammad, mwisho wa Manabii, pamoja na jamaa zake, Maswahabah wake wema, watwaharifu na wale waliowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
Ama baada ya hayo;
Hakika nimeulizwa zaidi ya mara mbili kuhusu hukumu ya kupaka juu ya soksi. Nimeelezwa sababu zilizolazimisha kuidhihirisha hukumu katika suala hili, kuieneza na kuitangaza kwa ummah kwa uwazi. Kabla ya hapo baadhi ya waalimu wa shule walilalamikia hali wanayokumbana nayo watoto na wasichana katika wudhuu´ wakati wa majira ya baridi kutokana na ugumu wa kuosha miguu na maumivu yanayowapata kwa sababu ya baridi kali. Vilevile matatizo yanayowapata masikini wakati wa baridi kwa sababu ya kuosha miguu yao. Nimeelezwa kuwa watoto wengi wa shule pamoja na vijana na wanawake hawaswali katika majira ya baridi kwa sababu ya maumivu ya kuosha miguu kutokana na maradhi yanayowapata miguu wakati wa baridi kama uvimbe, kukauka sana kwa ngozi na kutokea kwa vidonda. Na pia nilisimuliwa kuhusu tabu anayokumbana nayo msafiri katika meli za baharini na vyombo vya mvuke, endapo atataka kuosha miguu, na kwamba abiria wengi hawaswali kwa ugumu wa kuosha miguu katika mazingira hayo mawili.
Nimeelezwa yote hayo na nikaambiwa visa kadhaa vinavyoonyesha kuwa watu wengi huacha swalah kwa sababu ya kuacha kujifunza dini na kwa ujinga wao kuhusu ruhusa za Shari´ah iliyo imara. Nikaambiwa kuwa wangekuwa wanajua ruhusa inayowarahisishia mambo na kuwaondolea mzigo, basi wasingepata kisingizio cha kuacha swalah ambayo ni miongoni mwa nguzo kuu za imani na miongoni mwa alama mashuhuri za Uislamu. Kwa hiyo nilikuwa nikiwajibu wanaouliza kwamba dini ya Uislamu imejisitiri juu ya wepesi na kuondoa uzito katika hukumu zote na imefungua milango ya kurahisisha mambo kwa namna ambayo haipatikani wepesi zaidi yake. Kwa hivyo ikawa ni rehema na tiba ya yaliyo ndani ya vifua. Nilikuwa nikiwaambia kwamba, mbali na misingi iliyojengewa dini hii Tukufu ya wepesi na unyumbufu na kwamba msingi wa dini yake ni kuondoa uzito na kupanua mambo yanapokuwa magumu, basi suala hili la kupangusa juu ya soksi linajulikana vyema na ni lenye kutambulika kwa wanazuoni wote na pia limeelezwa wazi katika Hadiyth zilizopokelewa. Aidha ni madhehebu ya Maswahabah, wanafunzi wa Maswahabah, maimamu wenye kujitajidi na wapokezi wa Hadiyth kwa ujumla. Kwa hiyo hakuna udhuru kwa yeyote kulijua. Mwanafunzi asiyejali kulijifunza na kulitafuta, hali ni miongoni mwa masuala muhimu ya matawi ya Fiqh ambayo ummah unawajibika kuyajua. Hakuna elimu bila kujifunza na wala hakuna Fiqh bila kufahamu. Yule asiyetafuta elimu na wala asiyetia juhudi katika Fiqh na uelewa, basi yuko katika giza totoro na upotofu uliotanda. Hivyo basi hakuna uongofu isipokuwa kwa nuru ya Fiqh na elimu ya yakini. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Allaah anapomtakia mtu kheri basi humpa ufahamu katika dini.”[1]
Kisha nikaombwa nikusanye katika suala hili kitabu kidogo chenye manufaa na nikusanye humo Hadiyth zenye kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na masimulizi kutoka kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), wanafunzi wa Maswahabah na maimamu wanaotambulika. Matokeo yake nikamuomba Allaah chaguo zuri na kumuomba msaada, nikajitahidi katika kuchunguza yaliyopokelewa katika mada hii na nikayasoma kwa uchunguzi maneno mengi ya maimamu. Kisha nikakusanya katika kurasa hizi sehemu bora ya niliyoyasoma na kuyachunguza. Basi sifa njema zote njema ni za Allaah katika mwanzo na mwisho – Naye ni Mlinzi wa watu wema!
[1] al-Bukhaariy (71), at-Tirmidhiy (2645) na Ahmad (2790).
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 16-18
- Imechapishwa: 02/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 16-18
Imechapishwa: 02/04/2026
https://firqatunnajia.com/09-sababu-ya-kuandika-kitabu-al-mash-alaal-jawrabayn/