Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mkifunikwa na mawingu basi ikadirieni.”
Wanazuoni wametofautiana kuhusu maana yake:
1 – Ibaneni hesabu kwa namna ya kwamba kuufanya mwezi wa Sha’baan kuwa na siku ishirini na tisa na kufunga siku ya shaka. Haya ndio madhehebu ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah)[1]. Hilo ni kutokana na maneno Yake (Ta´ala):
وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ
“… na yule aliyebaniwa riziki yake… ”[2]
Kwa maana ya kwamba yule riziki yake imekuwa ngumu.
inayomaanisha kule kupungukiwa na riziki. Ikiwa mwezi mwandamo haukuonekana usiku wa siku ya thelathini ya Sha’baan kunahitaji upambanuzi. Ikiwa amezuiwa na mawingu au ukungu, basi kusifungwe. Vinginevyo watu wataamka wamefunga.
2 – Maana yake ni kuhesabu mwezi wa Sha’baan kuwa siku thelathini. Haya ndio maoni ya wengi wa wanazuoni katika Salaf na wale waliokuja nyuma[3]. Hilo linatiliwa nguvu na Hadiyth nyingine isemayo:
“Fungeni kwa kuonekana kwake na fungueni kwa kuonekana kwake. Ikiwa imefichika kwenu basi kamilisheni hesabu ya Sha’baan kuwa siku thelathini.”[4]
Maoni haya ndio ya sawa na ndio ambayo yanafanyiwa kazi na ndio maoni ya wakaguzi.
[1] al-Kaafiy fiy fiqh Imaam Ahmad (01/437) na ”al-Mughniy” (3/108) ya Ibn Qudaamah.
[2] 65:07
[3] Bidaayat-ul-Mujtahid (02/47), ”Majmuu’ Sharh-il-Muhaddhab (06/570), ”al-´Umdah fiy Sharh-il-´Umdah” (02/842) ya Ibn-ul-´Attwaar.
[4] al-Bukhaariy (1909).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/437)
- Imechapishwa: 23/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket