1- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho basi azungumze yenye kheri au anyamaze.”
2- Ni wajibu kwa aliye na akili kupambana na ulimi wake ili uzungumze yenye kheri. Ulimi unampelekea mtu katika uharibifu na kunyamaza kunampelekea mtu katika mapenzi na heshima. Anayeuhifadhi ulimi wake hustarehe. Ni bora kujirejea kwa kitu ambacho mtu amekinyamazia kuliko kitu alichokizungumza. Kunyazama ndio usingizi wa moyo na kuzungumza ndio uamkaji wake.
3- Maalik bin Anas amesema:
“Kila kitu mtu afaidike nacho kwa kupitiliza kwake. Isipokuwa tu maneno. Yanadhuru.”
4- Abuud-Dardaa´ amesema:
“Hakuna kheri yoyote katika maisha kama mtu hakuishi kwa kunyamaza na akaelewa au akazungumza ilihali ni mwanachuoni.”
5- Mwenye busara hatakiwi kuwashinda watu pindi wanapozungumza na asipingane nao. Hata kama kuzungumza ni utukufu katika wakati muafaka, kunyamaza katika wakati muafaka kuna ngazi ya juu zaidi.
6- Allaah (´Azza wa Jall) ameufanya ulimi kuwa juu ya viungo vingine vyote. Hakuna kiungo kinachochuma thawabu nyingi kama ulimi pindi utapokuwani wenye kutii. Na sijui vilevile kama kuna kiungo chenye kuchuma dhambi nyingi kama ulimi pindi unapoasi.
7- al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:
“Mambo mawili yanaufanya moyo kuwa mgumu; kuzungumza sana na kula sana.”
8- Sufyaan ath-Thawriy amesema:
“´Ibaadah inatangulizwa kwa kunyamaza, kisha kusoma, kisha kuyatendea kazi, kisha kuyahifadhi halafu kuyaeneza.”
9- al-Ahnaf bin Qays amesema:
“Kunyamaza kunaulinda ulimi kutokamana na kuyapotosha maneno, maneno ya hovyo na kuropokwa katika maneno. Vilevile kunampa heshima yule mwenye kunyamaza.”
10- Ni wajibu kwa mwenye busara kulazimiana na kunyamaza mpaka pale atapolazimika kuzungumza. Ni wangapi wamejuta kwa kuzungumza? Ni wangapi wamejuta kwa kukaa kimya? Hakuna khasara na wenye kujaribiwa sana kama wenye kuzungumza sana na walio na mioyo iliyofungamana.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 41-43
- Imechapishwa: 12/11/2016

Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 41-43
Imechapishwa: 12/11/2016
https://firqatunnajia.com/09-mwenye-akili-na-kunyamaza/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)